Watalaam
wa Masuala ya Nishati wakifuatilia
taarifa kuhusu masuala ya umeme wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la
Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Baadhi
ya Wataalam kutoka Tanzania
wakijadiliana jambo wakati wa mkutano huo.
Wataalam kutoka nchi mbalimbali wakijadiliana kuhusu masuala ya mafuta na gesi asilia wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Wataalam kutoka nchi mbalimbali wakijadiliana kuhusu
masuala ya Nishati Jadidifu wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Baadhi ya
Wataalam kutoka nchini Kenya wakijadiliana jambo.
Asteria Muhozya, Arusha
Wataalam wa Masuala ya Nishati
wanaoshiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki
unaondelea jijini Arusha wameibua
masuala kadhaa katika mkutano huo ambayo yanalenga kuharakisha utekelezaji wa miradi ya Nishati iliyokubaliwa na Jumuiya
hiyo.
Hayo yalibainika katika siku ya
Pili ya mkutano wa Timu ya Wataalam
kutoka Jumuiya hiyo ulioanza tarehe 30 Oktoba, 2017.
Mkutano wa Wataalam umefanyika
kabla ya kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 2 Oktoba, 2017 na kitafuatiwa na kikao
cha Mawaziri wa Nishati kinachotarajiwa
kuhitimisha mkutano huo tarehe 3 Oktoba,2017.
Baadhi ya miradi ya umeme
iliyojadiliwa ni pamoja na ile ya ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha Umeme
inayounganisha nchi na nchi ambayo
imeelezwa kuwa na kasi ndogo katika
utekelezaji wake.
Miongoni mwa miradi
hiyo ni pamoja na mradi wa Miundombinu ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 wa
Singida- Arusha- Namanga, mradi wa kV 220 wa Rusumo- Nyakanazi na mradi wa kV
400 wa Iringa- Mbeya - Tunduma.
Pia, Wataalam hao wamejadili
masuala ya kodi kwa vifaa vya umeme jua, miradi ya umeme ya mipakani ikiwemo
miradi ya Murongo/Kigagati na Nsogezi pamoja na Sera ya Usalama wa Nishati ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha, katika siku mbili za majadiliano,
Watalaam kutoka Jumuiya hiyo pia wamejadili masuala kadhaa yakiwemo yanayohusu nishati
jadidifu, gesi asilia na mafuta.
Kikao cha Makatibu Wakuu,
kitakachofanyika tarehe 2 Oktoba, kitatanguliwa na kikao cha Kamati ya Nishati cha Baraza hilo kinachofanyika leo tarehe 1 Oktoba, 2017 ambapo hoja
mbalimbali zilizoibuliwa na Wataalam hao zitajadiliwa katika kikao hicho.
Awali, akifungua mkutano wa
Baraza hilo kwa upande wa Wataalam tarehe 30
Oktoba, 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa
Sekta za Kijamii na Uzalishaji,
Christophe Bazivamo alieleza umuhimu wa nchi husika kuongeza kasi ya upatikanaji wa Nishati
miongoni mwa nchi wananchama ili kuwezesha mapinduzi ya Viwanda na kusisitiza
kuwa, miongoni mwa maeneo ya kipaumbele ya Jumuiya hiyo ni Nishati.
Bazivamo aliongeza kuwa, ili nchi hizo ziendeleee kiviwanda zinahitaji
nishati kwa kuwa ndiyo kichocheo kikuu cha maendeleo na kwamba, bado idadi
kubwa ya wananchi wa jumuiya hiyo haijaunganishwa na nishati ya umeme.
Pia, aliongeza kuwa, ukosefu wa
nishati hiyo siyo tu unadidimiza maendeleo ya watu pia unaathiri sekta ya elimu
kwa kuwa, kukosekana na nishati kunasababisha wanafunzi hususani waishio
vijijini kutumia muda mwingi kutafuta nishati ya kuni kwa ajili ya kupikia
badala ya kujikita na masomo.
Nchi zinazoshiriki mkutano huo ni
pamoja na Tanzania, Uganda, Rwanda, Uganda na Kenya. Aidha, Tanzania
inawakilishwa na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Wizara ya Maji, Mazingira na Nishati ya
Zanzibar, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Udhibiti
wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta , Zanzibar (ZURA).
Mwenyekiti wa Mkutano wa 12 wa
Baraza hilo ni nchi ya Uganda na Katibu
ni nchi ya Rwanda.





0 Comments