NA
WAMJW-DAR ES SALAAM.
WATUMISHI wa
kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha
huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi
katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.
“Tuna malengo
ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na
kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi
95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt.
Ndugulile amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa
kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya
wapatao 1600 mpaka hivi sasa.
Mbali na hayo
Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali
kupitia Wizara ya afya imetoa shilingi
milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.
“Tumetoa
milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400
kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na
milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema dkt. Ndugulile.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba dkt. Aloyce Musika amesema kuwa wahitimu
wanatakiwa kujiendeleza na elimu ili kuongeza kiwango cha elimu na kuwa
wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa uhakika nchini.
“Wahitimu
waliotunukiwa vyeti leo hii wasiwaze kuajiriwa tu bali wafikirie kuwa msaada wa
kutoa huduma za afya katika jamii huku wakifikiria kuongeza ujuzi zaidi katika
taasisi mbalimbali hapa nchini ili watoe huduma za afya kwa uhakika” alisema
Dkt. Musika
Mbali na hayo
msoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Saleh Said ambaye ni Muhitimu wa
fani ya Udaktari ngazi stashahada amesema kuwa anaiomba Serikali kuangalia kwa
ukaribu na kuweka utaratibu pindi wanafunzi wanapomaliza mafunzo yao kwenye
masula ya afya waweze kupata ajira kwa haraka.








0 Comments