Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea kwa mshtuko na masikitiko
taarifa za ajali ya moto kwenye ofisi za kituo cha Redio na Televisheni
cha Clouds Media cha Jijini Dar es Salaam hapo jana.
Waziri huyo ambaye yuko mkoani
Iringa kwa ziara fupi ya kikazi, ametoa pole kwa viongozi na
wafanyakazi wa kituo hicho cha redio na televisheni kwa kuunguliwa na
baadhi ya vifaa vya kazi vya chombo hicho cha habari na kuzitaka Taasisi
husika kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha moto huo.
Aidha, Dkt. Mwakyembe
amelipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kwa kuitikia wito na
kufika kwa haraka sehemu husika na hivyo kudhibiti moto huo usilete
madhara makubwa zaidi.
Imetolewa na:
Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
22/11/2017.

0 Comments