"Ofisi yangu ina jukumu la kutoa taarifa sahihi na kwa
wakati ya Serikali; Kusajili na kufungua Magazeti; Kusaidia Watu wa mifumo
mingine ya Serikali kusema" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Uhuru
wa vyombo vya habari upo wa kutosha. Serikali imeruhusu uhuru wa Vyombo vya
habari. Kuna Redio zaidi ya 150, tuna redio zaidi ya 30, kuna Magazeti zaidi ya
110 yanayotoka nchini" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Serikali
ina simamia Wananchi wapate habari sahihi na si kulishwa habari mbovu. Serikali
tunalisimamia hili" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Changamoto
iliyopo ni kuhakikisha habari zsahihi zinawafikia Watu wote kwa wakati" -
Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Rais
@MagufuliJP amefanikiwa sana kuleta mageuzi ya kifikra. Kujenga hari ya
Uzalendo, nidhamu, uwajibikaji kwa Watu wake wakiwemo Watumishi wa Umma na
Wananchi" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Rais
@MagufuliJP ameleta nidhamu kubwa ya matumizi ya fedha za umma. Mathalani
amefanikiwa kudhibiti safari za nje zisizo na tija" - Dk. H.A
@TZ_MsemajiMkuu
"Hapo
nyuma zilitumika bilioni zaidi ya 200 kwa safari tu wakati hivi sasa zimetumika
bilioni 25 tu kwa safari tumeokoa pesa nyingi"@TZ_MsemajiMkuu
"Rais
@MagufuliJP ameleta mageuzi ya kudhibiti Wafanyakazi hewa zaidi ya 20,000 na
kuokoa zaidi ya Tsh. Bilioni 238. Ni mageuzi makubwa" - Dk. H.A
@TZ_MsemajiMkuu
"Tumeondoa wafanyakazi hewa takribani elfu 20 kwa zoezi
hilo tumeokoa bilioni 238" @TZ_MsemajiMkuu
"Hawa
wanaopiga kelele juu ya mageuzi ya rasilimali za madini. Ipo siku watanyamaza
wakiona manufaa ya wazi. Serikali ya @MagufuliJP imeonyesha uzalendo kwenye
madini" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Zipo
nchi kubwa duniani awapati 50/50 kwenye Madini sisi tumeweza @TZ_MsemajiMkuu
"Serikali
itaendelea kuhakikisha kila kilicho chetu tunakipata"@TZ_MsemajiMkuu
"Kwenye
vyeti feki Serikali ya Rais @MagufuliJP imeokoa zaidi ya Tsh. Bilioni 148
ambazo zinaenda kwenye shughuli za kimaendeleo." - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Sekta
ya habari ni sekta nyeti na Sheria hii ya habari tuliyo nayo sasa imeleta
maboresho na ubora kwenye sekta ya habari nchini" - Dk. H.A
@TZ_MsemajiMkuu
"Huwezi
kutoa habari kwa kuingilia faragha ya mtu" @TZ_MsemajiMkuu
"Huwezi
ukakiacha kituo cha radio kinawachochea wakulima wakawaue wafugaji arafu
ukasema wana haki ya habari "@TZ_MsemajiMkuu
"Sheria
mpya ya huduma ya habari vimeweka ustawi wa vyombo vya habari na si kweli ipo
kwa ajili ya kufungia habari." - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Popote
duniani hakuna nchi yenye sheria inayosema andika chochote"
@TZ_MsemajiMkuu
"Hakuna
nchi yeyote Duniani inayotoa Uhuru kwa vyombo vyao vya habari kuwa na uhuru wa
kuandika chochote kile wanachojisikia" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Uandishi
wa habari ni taaluma sasa ukikiuka sisi kama serikali hatuwezi
kukuacha"@TZ_MsemajiMkuu
"Sisi
tunailea sekta yote ya habari"@TZ_MsemajiMkuu
"Wananchi wapuuze habari kuwa Serikali inafungia vyombo vya habari
inapojisikia bali ina zingatia sheria" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Chombo
cha habari kinatakiwa kifuate miiko"@TZ_MsemajiMkuu
"Vijana waamue kufanya kazi, wawe Wazalendo, wamwogope
Mungu. Safari ya Mabadiliko ni ngumu lakini inahitaji uvumilivu" - Dk. H.A
@TZ_MsemajiMkuu
"Watanzania
wamuunge mkono Rais @MagufuliJP atimize utekelezaji wa ilani ya uchaguzi"
- Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Mwakani
2018 mwezi Julai Serikali italeta ndege kubwa ya kisasa itakayokuwa inakwenda
popote pale Duniani" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
Mheshimiwa
Rais @MagufuliJP alikuta mikopo inatolewa kiasi cha bilioni 48 kwa mwaka Lakini
sasa hivi tumefikia bilioni 472 @TZ_MsemajiMkuu
"Fedha
zipo na watapata kila mwanafunzi mwenye haki ya kupata"@TZ_MsemajiMkuu
"Serikali
ya Rais @MagufuliJP inatoa Tsh. Bilioni zaidi ya 400 kwa Wanafunzi. Kwa mara ya
kwanza fedha imetangulia vyuoni kabla ya Wanafunzi kuanza masomo" - Dk.
H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Serikali
imeboresha makusanyo kutoka Tsh. Trilioni 9.9 mpaka Tsh. Trilioni 14 kwa
mwaka" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
Mheshimiwa
@MagufuliJP alipoingia madarakani tulikuwa tunakusanya kodi kwa kiasi cha
"Trilioni 9.9.Leo hii tunakusanya trilioni 14 kwa mwaka haya ni mafanikio
makubwa"@TZ_MsemajiMkuu
"Serikali
imeleta miradi ya kihistoria nchini ya kuzalisha umeme kupitia miradi ya
Kinyerezi 1 & 2" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Hivi
tunapozungumza kuna watu hawalali kuna watu wanajenga reli Usiku na
mchana"@TZ_MsemajiMkuu
Dk.
Hassan Abbas ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari na Maelezo na Msemaji Mkuu wa
Serikali aliyasema hayo katika kipindi cha VijanaTz kilichorushwa Mubashara
siku ya Ijumaa Novemba 10, 2017 kupitia mitandao ya kijamii ya UVCCM ya
Twitter, Facebook na Instagram
IMEANDALIWA
NA;
Idara
ya Uhamasishaji na Chipukizi
UVCCM Taifa
0 Comments