Msanii wa muziki wa bongo fleva Harmorapa amefunguka na kusema
kuwa katika mwaka 2017 amehangaika kulipata penzi la mwanadada Wema Sepetu
kiasi cha kuamua kwenda kwa mganga wa kienyeji mara tatu ili aweze kumpata
mrembo huyo.
Harmorapa akiongea kwenye kipindi cha eNewz cha EATV
amedai kuwa baada ya kuhangaika kwa marafiki zake Wema Sepetu na kugonga mwamba
aliamua kwenda kwa babu (mganga) ambapo amedai kwa mara ya kwanza aliambiwa
apeleke kuku mweupe, na alipeleka huyo kuku lakini aliporudi mjini Dar es
Salaam mambo yake yakawa bado vile vile.
"Nimemuendea kwa babu Wema Sepetu mara tatu, nilipokwenda
mara ya kwanza niliambiwa nipeleke kuku mweupe, nikapeleka zangu yule kuku
mganga akafanya yake lakini niliporudi mjini sikuona mabadiliko yoyote yale,
nikamfuata tena babu akaniambia nipeleke vitu vingine viwili ambavyo hapa
nashindwa kuvisema" alisema Harmorapa
Harmorapa aliendelea kufunguka jinsi ambavyo amehangaika
kulitafuta penzi la Wema Sepetu na kudai ilifika wakati aliambiwa apeleke
mchanga wa unyayo wa Wema Sepetu au mchanga ambao mwanadada huyo ametemea mate,
kitu ambacho Harmorapa amedai kilikuwa kigumu sana kwake kwa sababu hapati
nafasi ya kukutana live na Wema Sepetu.
Hata hivyo Harmorapa kwa sasa amesema amemwachia Mungu juu ya
jambo hilo baada ya kuona harakati za kwa mganga wa kienyeji zinakwama.

0 Comments