Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo
akifafanua jambo wakati akiongea na Waaandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa
kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa Mikutano wa
Tamisemi Mjini Dodoma.
Baadhi ya
waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo kwenye mkutano i
kuhusu matokeo ya uchaguzi wa
wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika ukumbi wa
Mikutano wa Tamisemi Mjini Dodoma.
Angela Msimbira –
OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema
kati ya wanafunzi 662,035 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya
msingi wanafunzi 650,862 sawa na asilimia 98.31
wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2018
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018
Tanzania Bara kwenye kikao na waandishi wa habari leo katika ofisi za Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Jafo amesema kuwa idadi wa
wanafunzi mwaka huu imeongezeka kwa wanafunzi 124,209 ambapo ni sawa na
asilimia 23.58 ikilinganishwa na
wanafunzi 526,653 waliochaguliwa awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza
mwaka 2016.
Amesema
kuwa wanafunzi 1912 wenye uhitaji maalum (pupils with special needs) waliofaulu
mitihani ya darasa la saba
wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018
kwenye shule za sekondari za Serikali.
Mhe.
Jafo amefafanua kuwa wanafunzi 11,173
sawa na asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ya uchaguzi
kutokana na uhaba wa miundombinu
ya elimu hususani vyumba vya madarasa
kwenye baadhi ya Halmashauri ya Mikoa ya
Lindi (170), Mbeya (3,092), Rukwa (4,091), Manyara (1,268), Katavi (976) na
Simiyu (1,576).
Amesema
kuwa Halmashauri ambazo zimeshindwa kuwapangia wanafunzi wote waliofaulu nafasi
ya kujiunga na kidato cha kwanza ni Halmashauri za Lindi wanafunzi (80) Mbeya
(207),Halmashauri ya Jiji la Mbeya ( 1,227), Mbarali (1,578), Kalambo (166), Nkasi (1,318), Halmashauri ya
Wilaya ya Sumbawanga (1,054),
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
(1,553), Babati (581). Hanang (687), Mpanda (262), Nsimbo (714), Halmashauri ya
Mji wa Bariadi (369) na Halmashauri ya Wilaya ya Busega (1,207).
Mhe.
Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa ambayo haijakamilisha ujenzi wa miundombinu hasa
ya vyumba vya madarasa kuhakikisha
wanakamilisha hadi kufikia mwezi februari, 2018 ili wanafunzi watakaochaguliwa
kwenye awamu ya pili wapate nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018.
“Lengo
la Serikali ni kuhakikisha kuwa
wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi ya kujiunga
na masomo ya kidato cha kwanza
nimeshatoa maelekezo kwa wakuu wa
mikoa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka
2018” Amesema Jafo
Mhe.
Jafo amesisitiza kuwa walezi na
wanafunzi ambao watakosa nafasi katika
awamu ya kwanza ya uchaguzi kuwa
wavumilivu wakati mikoa inajiandaa kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wote kuanza
na masomo ya kidato cha kwanza.
Amewaagiza waalimu
na watendaji wa elimu katika
ngazi zote nchini kuongeza bidii katika
usimamiaji na ufuatiliaji wa utoaji wa elimu nchini na kushirikiana na wadau wa
elimu kukamilisha majengo na kuandaa
mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha
kwanza 2018 bila vikwanzao vikiwemo
michango na ada ili kutekeleza sera ya
utoaji wa elimu msingi bila malipo.
Aidha
amewaomba Wazazi, Walezi na jamii kwa ujumla kushirikiana na Wilaya,
Halmashauri na shule, kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliochaguliwa wanaandikishwa , wanahudhuria
na kubaki shuleni hadi
watakapohitimu elimu ya Sekondari.


0 Comments