Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya
nchini Australia wakifanya upasuaji kwa mtoto
ambaye vyumba vyake vya moyo
havijakamilika na hivyo damu kwenda kwa wingi kwenye mapafu katika kambi ya
siku tano ya matibabu ya moyo iliyomalizika leo katika Taasisi hiyo.
Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na mishipa
ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini
Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji
wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery
Bypass Grafting) katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo
iliyomalizika leo katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 16 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri kati ya hao watoto ni tisa na
watu wazima saba.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Open Heart
International ya nchini Australia Russel Lee akiongea na waandishi wa Habari
kuhusu upasuaji wa moyo wa mtoto ambao umekaa upande wa kulia na mishipa yake
ya damu chafu na safi imeingiliana katika upasuaji huo wameweza kulinda mapafu
yalikuwa yanapokea damu kwa wingi kutoka
kwenye mishipa ya moyo na mtoto kawekewa kifaa ambacho kitamsaidia moyo wake
kufanya kazi vizuri (Pace Maker). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Daktari Bingwa
wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau.
Picha na JKCI

0 Comments