Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kulia), akipokea Salamu ya
Heshima kutoka kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu
Mwandamizi wa Uhamiaji Muhsin A. Muhsin akimkaribisha rasmi Kamishna,
kutembelea Kituo cha Uhamiaji kilichopo Bandari ya Mkokotoni, Wilaya ya
Kaskazini “A” jana tarehe 06 Disemba, 2017 wakati akiendelea na ziara ya
kikazi Mkoani Humo.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (juu), akiwaasa watumishi wa
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, kuzingatia Maadili ya kazi,
Heshima na Uadilifu kuwa ndio nguzo kwa Utumishi uliotukuka. Pia
alikemea vitendo vya Rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wasio
waadilifu. Alitoa nasha hizo leo tarehe 07 Disemba, 2017 wakati
akihitimisha ziara ya siku tatu Mkoani Humo. Kulia kwake ni Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji,
Muhsin A. Muhsin na kushoto ni Afisa Utumishi, Mrakibu wa Uhamiaji, Ali
J. Abdulkadir.
Afisa
Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji,
Muhsin A. Muhsin akiwasilisha kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari
Masoud Sururu, taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi hiyo kuanzia Julai hadi
Novemba, 2017. Huku akitilia mkazo ongezeko la makusanyo ya maduhuli ya
Serikali kwa kipindi hicho Dola za Kimarekani 34,000$ zilikusanywa.
Alitoa taarifa hiyo leo tarehe 07 Disemba, 2017 wakati Kamishna Sururu
akihitimisha ziara ya siku tatu Mkoani Humo.
Koplo
wa Uhamiaji, Mosi Shadhil Khatib akichangia hoja zilizojadiliwa katika
Kikao cha Pamoja cha Wafanyakazi wote wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini
Unguja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, Leo
tarehe 07 Disemba, 2017 wakati alihitimisha ziara ya kikazi ya siku tatu
Mkoani humo.
Mkuu
wa Bandari ya Mkokotoni, Bwana Ahmed Salim Said, akimuonesha Kamishna
wa Uhamiaji Zaznibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa aliombatana nao,
eneo linalotumiwa na baadhi ya Manahodha kushusha abiria kinyume na
utaratibu wa Bandari hiyo, wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye
maeneo ya utendaji kazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja
jana tarehe 06 Disemba, 2017.
Sheha
wa Shehia ya Mnarani Bwana Mdungi Sharifu Makemi akimuonesha Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa alioambatana nao,
eneo lenye changamoto kubwa wanazokabiliana nazo za Uingiaji wa watu
wasiofata sheria katika Ukanda huo. Alipofanya
ziara ya kikazi kwenye maeneo ya utendajikazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa
wa Kaskazini Unguja jana tarehe 06 Disemba, 2017
Sheha
wa Shehia ya Nungwi – Banda Kuu Bwana Mohamed Khamis Haji, akimuonesha
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa
alioambatana nao, eneo lenye changamoto kubwa wanazokabiliana nazo za
Uingiaji wa watu wasiofata sheria katika Ukanda huo. Alipofanya
ziara ya kikazi kwenye maeneo ya utendajikazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa
wa Kaskazini Unguja jana tarehe 06 Disemba, 2017
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kulia), akimsikiliza kwa
makini Sheha wa Shehia ya Kilindi Bwana Omar Ali Mussa (wa pili
kushoto), akitoa shukran zake kwa Uongozi wa Idara kwa ushirikiano
mkubwa anaoupata toka kwa Askari wa Uhamiaji.
Akisisitiza kauli hiyo
Sheha alisema “Ziara yako Kamishna imethibitisha kauli yangu na
umeonesha kwa vitendo jinsi ulivyojipanga kushirikiana na wananchi wa
eneo letu kutatua changamoto za baadhi wageni wanaoishi hapa bila ya
kufata utaratibu” aliyasema hayo jana wakati Kamishna akiendelea na
ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Unguja.









0 Comments