Katika kusherehekea
sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya, kampuni ya simu TECNO mobile
Ltd imeandaa sherehe za awali za Krisimasi maalumu kwa wadau wake.
TECNO iliwakutanisha
wadau na mashabiki wake kutoka katika mitandao ya kijamii mbalimbali ikiwemo,
Twitter, Instagram, Facebook na TECNO spot katika hafla fupi iliyopewa jina la
“TECNO Fans Night” iliyofanyika katika uwanja wa burudani wa ESCAPE ONE Mikocheni.
Kusudio likiwa ni
kuwapongeza na kutoa shukurani kwa wadau na mashabiki kwa kuwa pamoja na
kampuni hiyo kwa mwaka mzima na kuwa mabalozi wa kampuni hiyo ya simu.
Sherehe hiyo ilikua na
ugeni wa mtangazaji maarufu afahamikae kwa jina la “Lil Ommy” Omary Tambwe wa
Times FM akiwa kama shereheshaji wa sherehe hiyo iliyoandaliwa na TECNO. Hafla
hiyo ilipambwa kwa michezo, burudani na chakula cha jioni
huku zawadi mbalimbali zikitolewa kwaaajili ya mshabiki na
wadau wa kampunI hiyo ya TECNO waliofika.
“Kiukweli nimefurahi kuwa
hapa, kuungana na wenzangu. Nimepata nafasi ya kuongeza marafiki usiku wa leo,
asante sana TECNO” – alisema mmoja wa wadau/shabiki wa TECNO.
“Mpaka sasa kwa mwaka huu
tumeweza kuwa na ushawishi sana kwa upande wa mitandao ya kijamii na tumeweza
kuwapa kile wadau na mashabiki wetu wanapenda, nahisi ndicho kilichoweza kutupa
mabalozi kama hawa. Kiukweli hatuwezi kuwa sisi bila ya watu kama hawa ambao
waipenda bidhaa na kampuni hivi, hivyo ni sawa tu kama na sisi kama kampuni
tukatenga muda ili kuweza kuungana nao kusherehekea mafanikio na pia sikukuu” –
Meneja mahusiano.
TUNAWATAKIA KHERI YA
KRISIMASI
Tazama video ya yaliojiri



0 Comments