Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
...............
NA TIGANYA VINCENT RS TABORA
SERIKALI ya Mkoa wa
Tabora imeziagiza Halmashauri zote kuanza upandaji wa miti ya matunda 6,000
kila moja katika Taasisi na Shule na miti isiyo ya matunda ili kutekeleza agizo
la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Agizo hilo limetolewa
jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akizindua awamu ya pili ya
upandaji miti kwa Wilaya ya Igunga ambapo miti 280 ilipandwa.
Mwanri alisema kuwa
miti hiyo ni sehemu ya miti milioni na laki tano (1,500,000) kwa kila
Halmashauri kila mwaka iliyoagizwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Alisema kuwa kila
Halmashauri ni lazima pamoja na kupanda miti ya aina nyingine ianze kupanda
matunda katika Shule mbalimbali na Taasisi kama vile Hospitali kwa ajili ya
kuwasaidia wanafunzi na wagonjwa.
Mkuu huyo wa Mkoa
alisema kuwa kila siku anahitaji apate taarifa na takwimu kuhusu maeneo ambapo
miti imepandwa na kiwango chake kwa siku.
Aidha Mkuu wa Mkoa
amewaagiza Wakurugenzi Watendaji wote kusimamia Sheria za Mazingia ili
kukabiliana na waharibifu katika mistu mbalimbali ikiwemo wakati ovyo miti.
Alisema kuwa hatua hiyo
itasaidia kurejesha uoto wa asili na viumbe wengine ambao walikwishaanza
kutoweka kutokana na uharibifu wa mistu.
Katika hatua nyingine
Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza kuhakikisha wanapanga matumizi mazuri ya ardhi kwa
ajili ya shughuli za kilimo, huduma za jamii, ufugaji , mistu na uwekezaji.
Kwa upande wa Mkuu wa
Wilaya ya Igunga John Mwaipopo alisema kuwa hatamuonea huruma mtumishi au
mwananchi yoyote atakayekaidi zoezi la upandaji wa miti katika eneo hilo.
Aliongeza kuwa hivi
wanaendelea na zoezi kukamata mifugo yote inayozurura mjini na kuharibu miti na
wahusika kutozwa adhabu.
Mwaipopo alisisitiza
kuwa lengo lao ni kutaka uoto wa asili katika Wilaya ya Igunga unarejea na
kuwavutia watu wengi kwenda kuangalia madhari ya kuvutia.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Igunga Revocatus Kuuli alisema kuwa hadi hivi
wameshatumia kiasi cha milioni 15 katika zoezi la upandaji miti.
Alisema kuwa
wataendelea kupanda katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo ili kurejesha
mimea ya asili ya eneo hilo.
Hadi jana jumla ya miti
3,233 ilikuwa imepandwa na Halmashauri mbalimbali isipokuwa Urambo ndio ilikuwa
haijapanda

0 Comments