Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa
Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la
Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.
January Makamba akitoa maelezo ya kampeni ya kupanda miti wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa
Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la
Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiandaa mti wake kabla ya kuupanda mara baada ya kuzinduzi kampeni ya kuufanya mji wa
Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la
Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipanda mti mara baada ya kuzinduzi kampeni ya kuufanya mji wa
Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji bonde la
Makutupora, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan ameagiza kuwa kampeni ya kupanda na ustawishaji miti isiishie
Dodoma mjini tu bali ienee katika Wilaya zote za mkoa wa huo na hatimaye nchi
nzima.
Makamu wa Rais aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya
kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani.
Makamu wa Rais alisema upandaji miti si kwa ajili ya
kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi, kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi ambapo alitolea mfano mti
mmoja uliokomaa unaweza kunyonya hadi kiasi cha kilo 150 za gesi ya hewa ya
ukaa kwa mwaka,husaidia kupunguza joto, kusaidia kuboresha afya zetu za mwili
na akili kama tafiti zinavyoonyesha .
“Ni dhahiri, kampeni hii ya kuifanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani ni
kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo
Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kwa vitendo.” Alisema Makamu
wa Rais.
Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Wana Dodoma kuipokea
kampeni hii kwa mikono miwili na kutoa kila aina ya ushirikiano ili kufikia
lengo zuri lililokusudiwa.
Makamu wa Rais ambaye alihamia rasmi mjini Dodoma siku ya ijumaa
tarehe 15 Desemba, 2017 alitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Ofisi yake kwa kuja na wazo
zuri .
Makamu wa Rais alisisitiza kuwa hategemei kuona zoezi la
upandaji miti lianze na kuisha leo, na badala yake liwe la kudumu, pia
alizitaka manisapaa zitunge sheria ndogo zitakazoelekeza shule, chuo, taasisi na
familia kuanzisha bustani ndogo za miti
zitakayomudu mazingira husika,Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa ni vyema
kupunguza ukataji wa miti kiholela ambapo alizitaka sheria, kanuni na taratibu zizingatiwe
kabla ya kukata miti na kusema tupande miti kabla ya kukata mti.
Makamu wa Rais alimalizia kwa kutoa shukrani kwa kampuni ya
TATU Mzuka kwa kujitoa na kuhakikisha kampeni hii inatekelezwa na kutoa wito
kwa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania iige mfano na kuelekeza
makampuni mengine ya bahati nasibu yaweze kutoa mchango wake katika shughuli za
kijamii hususan kwenye suala la hifadhi ya mazingira.
Pia Makamu wa Rais alitoa shukrani kwa Jeshi la Kujenga
Taifa Makotopora, DUWASA, Magereza na Tanzania Forest Services (TFS) kwa
kujitoa na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hili.
Mwisho, Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wa mkoa wa Dodoma
kuanzisha vikundi mbali mbali vya upandaji .





0 Comments