MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akifungwa
kiskafu na Vijana wa Chipukizi wa Mkoa wakati wa mapokezi yake
alipowasili katika Viwanja vya Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amaan
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib, alipowasili katika
viwanja vya Afiisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakati wa mapokezi yake
BAADHI ya Wanachama wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar wakiwa katika
ukumbi wa Mkutano Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakimsikiliza Makamu
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa
hafla ya mapokezi yake Zanzibar
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia
Wanachama wa CCM katika hafla ya mapokezi yake yaliofanyika katika Afisi
Kuu ya CCM MKoa wa Mjini Amaan Zanzibar. baada ya kuwasili akitokea
Dodoma wiki iliopita baada ya kuchaguliwa kwa mara ya Pili kushika
nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura nyingi katika
mkutano Mkuu wa Tisa wa CCM uliofanyika Dodoma.
Picha Ikulu
…………..
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM), Mwekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein
amewataka viongozi wa chama kutosita kuwajadili wanachama ambao
wanakiuka maadili ya chama hususan vitendo vya rushwa.
Pia, amesema wanachama hao
wakishajadiliwa hawatasita kufukuzwa ndani ya CCM na kwamba imefikia
hatua baadhi ya watu hao ambao wanafanya vitendo hivyo wanaonewa haya.
Hayo ameyasema leo , katika
sherehe za kumpongeza kuchaguliwa tena nafasi ya Makamu Mwenyekiti,
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa Mjini ,ambapo aliwataka
viongozi hao kutofumbia macho vitendo hivyo ndani ya CCM.
katika maongezi yake Dk.Shein
ameongeza kuwa vitendo hivyo vya rushwa si jambo jipya ndani ya CCM na
kwamba inaharibu sana maadili ya chama.
“Vitendo hivi vya rushwa ndani ya
CCM si suala jipya lakini tunaoneana huruma, tunafichiana na baadae
tunalalamikiana wakati chama ni ya wanachama hivyo lazima
tushirikiane,”amesema.
Makamu Mwenyekiti huyo Dk.Shein
amesema utaratibu wa chama kinajielekeza wanachama ambao wanakiuka
maadili wanapaswa kujadiliwa kuanzia ngazi za tawi na baadae
inawasilishwa kwenye uongozi wa juu na kuchukuliwa hatua.
Ameeleza chama kipo kwa wanachama
ikiwemo kwenye mashina na matawi na taratibu zinafafanua kuwa ngazi hizo
ndipo mambo hayo yanazungumzwa kwamba mwanachama akikiuka maadili
anajadiliwa kwenye tawi.
“Anajadiliwa kwenye kamati ya tawi
na shina, kamati ya jimbo, kamati ya wilaya, Halmashauri ya wilaya
ndipo wanapojadiliwa huku kwamba anafaa ama hafai hachukuliwe hatua za
kufukuzwa ama asichukuliwe,”amesema.
Makamu Mwenyekiti huyo amesema
utaratibu unaeleza kuwa baada ya kujadiliwa wanachama hao taarifa
itapelekwa kwenye ngazi za juu na kufanya maamuzi ya kumfukuza.
“Nachotaka kueleza kuwa kazi hii
ni ya wote na kwamba jukumu kubwa ni kuhakikisha CCM inashinda mwaka
2020 msiwafiche watu ambao wanataka kuharibu chama, na kwa kufanya hivyo
ni sawa na kuwa ndumi la kuhili tunayoyasema sio tunayoyafanya,”amesema
Makamu Mwenyekiti.
Amefafanua kuwa kazi ya siasa ya
kipindi hiki lazima kuongeza kasi ambapo kuna mambo zaidi ya kuyafanya
na hata Mwenyekiti Dk.John Magufuli alisisitiza kwenye mkutano mkuu
uliofanyika Desemba 18, mwaka huu mjini Dodoma.
Mbali na hilo, Dk.Shein amewataka
viongozi wa serikali kutambua na kuheshimu CCM kutokana na kuwa
wanafanya kazi ya utekelezaji wa chama hivyo hawanabudi kukithamni.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar, Dk.Abdallah Juma Saadalla(Mabodi), amesema wanachama kutoka
visiwani humo wanatarajia kusimamia vyema ibara ya tano ya kuhakikisha
CCM inashinda mwaka 2020.
Ameongeza kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa na mawimbi makubwa sana lakini watu walioshiriki walikuwa wanastahili.
“Bado tunafanya juhudi za kutoa
elimu kwa viongozi wa chama kuhusu suala la kuzingatia kanuni na maadili
ili kuhakikisha wanasongesha gurudu la uchaguzi wa mwaka 2020″amesema.
Dk.Mabodi ameeleza kuwa
anamshukuru Mungu kwa kuwa wagombea wote ambao wamepita kwenye uchaguzi
huo asilimia kubwa wana maadili ya kutosha.




0 Comments