Random Posts

Matukio katika picha kufungwa kwa kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya  akikabidhiwa  ngao na mwenyekiti mtendaji wa Taasisi ya Kiislam ya DHI NUREIN Sheikh Said Abri ya kuishukuru Serikali kuwezesha kufanyika kwa kambi ya upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua uliofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Msaada ya Muntada ya nchini Uingereza  kupitia  mradi wake wa afya wa  Little .
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea ngao ya shukurani   kutoka kwa Mkurugenzi  wa Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao  Makuu mjini London nchini Uingereza Hamid Azad  katika hafla fupi ya kufunga kambi ya upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua kwa watoto iliyomalizika leo. Jumla ya watoto 131 walifanyiwa uchunguzi kati ya hao  54 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na 28 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi  akimpatia cheti  cha kumshukuru Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya DHI NUREIN Shams  Elmi katika hafla fupi ya ufungaji wa kambi ya upasuaji wa Moyo kwa watoto wa  kufungua kifua na bila kufungua kifua uliofanywa na  Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Muntada kupitia mradi wake wa afya wa Little Hearts . Taasisi ya DHI NUREIN ndiyo iliyoratibu kufanyika kwa kambi hiyo ya matibabu hapa nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa katika  picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete,  Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao yake  Makuu yake mjini London nchini Uingereza na wafanyakazi wa mradi wa  Little Hearts kutoka nchini Saudi Arabia mara baada ya kufunga kambi ya upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua kwa watoto iliyofanyika tarehe 9/12/2017 hadi  15/12/2017.

Picha na JKCI

Post a Comment

0 Comments