Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili
kushoto) akitazama hatua ya uchomaji wa Madini ya Jasi kwenye kiwanda cha
kampuni ya mzawa cha RSR kilichopo katika Kijiji cha Sanjaranda, Itigi kabla ya
kusagwa kuwa unga na baadaye kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa ajili ya
kuuzwa na mwingine kutumika katika Kiwanda cha kutengenezea mapambo ya
Majumbani, katika kiwanda kilichopo Singida mjini.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto)
akiwasikiliza wachimbaji na wafanyakazi wa machimbo ya Jasi, yaliyopo katika
Kijiji cha Kihanju, Itigi, Mkoani Singida alipofanya ziara kwenye machimbo
hayo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia)
akishuhudia upakiaji wa Madini ya Jasi katika kijiji cha Kihanju, Itigi yanayosafirishwa
kuelekea kwenye Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement ikiwa ni moja ya malighafi
ya kutengenezea Saruji.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili
kulia) akikagua mitambo ya kusagia mawe ya Madini ya Jasi kwenye Kiwanda cha kutengeneza
Chaki cha Dobercolor kilichopo katika Kijiji cha Majengo, Itigi.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili
kulia) akimsikiliza Meneja wa kiwanda cha kutengeneza Chaki cha Furaha, kilichopo
katika Kata ya Tambukareli, Itigi, Peter Nolasco (kulia) akielezea namna Madini
ya Jasi yanavyosagwa na kuwa unga (Gypsum powder) kwa ajili ya kutengenezea
Chaki.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akitazama
Chaki zinazozalishwa na Kiwanda cha Dobercolor kilichopo katika Kijiji cha
Majengo, Itigi ambazo huuzwa ndani na nje ya Mkoa huo huku lengo likiwa ni
kuuza nje ya Tanzania.
.............
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo hapo jana alifanya ziara kwenye machimbo ya
Jasi (Gypsum) ya Mkoani Singida na kuzungumza na Wafanyabiashara na Wachimbaji wa
Madini hayo ambapo aliwahakikishia ushirikiano wa dhati wa kufikia malengo
waliyojiwekea.
Alitembelea
maeneo ya machimbo ya Madini ya Jasi na Viwanda vidogo vya uongezaji thamani ya
madini hayo ikiwemo viwanda vya kusaga madini ya Jasi ambayo unga wake
unasafirishwa nje ya Mkoa huo, viwanda vya kutengeneza chaki vilivyopo Itigi na
kiwanda cha utengenezaji wa mapambo ya majumbani kilichopo Singida Mjini.
Naibu
Waziri Nyongo yupo Mkoani Singida kwenye ziara ya siku Tatu ya kutembelea
maeneo mbalimbali ya uchimbaji wa madini Mkoani humo ili kujionea shughuli
zinazofanywa kwenye maeneo hayo na kuzungumza na wachimbaji wa madini ili kubaini
changamoto zinazowakabili kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wake.
Kwa
mujibu wa wachimbaji wa madini hayo, Madini ya Jasi hutumika kwa matumizi
mbalimbali ikiwemo kutengenezea chaki, hospitalini kwa watu waliovunjika na
kutengeneza viungo bandia, kutumika kutengenezea saruji, urembo majumbani,
hutumika kama insulation kwenye
majengo makubwa kwa kuwa Jasi huzuia moto, kutengenezea midoli na masanamu,
kutengeneza meno bandia na pia hutumika kama mbolea
0 Comments