Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Japhet Hasunga ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
ianze mchakato wa kuandaa sheria ya kutoka Wakala kuwa Mamlaka ya
Usimamizi wa Misitu Tanzania ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa
vile ikiendelea kubaki kuwa Wakala kuna baadhi ya mambo itashindwa
kuyashughulikia
Wakala
ni Idara za Serikali zilizoondolewa kwenye serikali kuu na zina nusu mamlaka na
hazina mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake zenyewe.
Amesema
uanzishwaji wa Mamlaka hiyo itasaidia kupunguza migongano kati ya misitu iliyo
chini ya Tamisemi pamoja na vijiji kwa vile kutakuwa na Mamlaka moja
ya kusimamia misitu tofauti na ilivyo sasa.
Ameyasema
hayo jana wakati akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani
(TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam
Amesema
TFS kwa hatua iliyofikia kwa sasa haistahili kuwa Wakala kutokana
na kazi kubwa iliyonayo hivyo inahitaji kuwa Mamlaka ili iweze kutekeleza
majukumu yake kwa uhuru zaidi.
Wakati
akizungumza na Watumishi, Naibu Waziri Hasunga amemtaka Mtendaji Mkuu wa
TFS, Dos Santos Silayo ahakikishe katika mpango mkakati
utakaoandaliwa hivi sasa suala la uanzishwaji wa Mamlaka lipewe
kipaumbele.
Katika
hatua nyingine, Ameiagiza TFS iunde chombo cha kusimamia na
kudhibiti ubora wa mazao ya misitu.
Amesema
chombo hicho kitakuwa kikipanga mazao ya misitu kulingana na ubora wake na sio
kama sasa inavyofanyika mbao zozote zile zimekuwa zikiuzwa sokoni pasipo
kujali ubora wake.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza
na Watumishi wa Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam jana . Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos
Silayo.
(Picha na Lusungu Helela-MNRT)
Amesema
kuna changamoto ya bei za mbao sokoni na pia kuna changamoto ya ubora wa
mbao zilizoko sokoni, Mbao nyingi zimetengenezwa kwa miti ambayo
imevunwa ikiwa na miaka sita au kumi ni lazima ubora wake uwe
hafifu.
‘’
Halafu unaenda kumshindanisha na mtu anayeuza mbao ambazo miti yake imevunwa
ikiwa na miaka 18 haziwezi kushindanishwa ubora kati ya mbao
hizo lazima kiwepo chombo cha kuthibiti kama vile kwenye chakula kuna TFDA na
kwenye bidhaa kuna TBS’’ alisema
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri Hasunga amemtaka kila mtumishi ahakikishe
anapambana na rushwa kwa kumuagiza Mtendaji Mkuu wa TFS Prof.
Silayo kuwahamisha watumishi pale inapotokea fununu kuwa mtumishi
fulani anajihusisha na rushwa hata kama bado haijathibitika kwa vile fununu
hizo haziwezi kuanza tu bila ya kuwa harufu ya mazingira ya kupokea
rushwa yanayotengenezwa.
Amesema
katika suala la ugawaji wa vitalu kuna vitendo vya rushwa vinafanyika
kwani baadhi ya watu wanapewa vibali vya kuvuna kwa muda wa miezi minne lakini
uvunaji ule unaendelea kwa muda wa mwaka mmoja wakati ilitakiwa
kitalu hicho kivunwe kwa muda wa wiki mbili tu.’’ Alisema
‘’Mimi
sikurupuki kwenye maamuzi yangu na sio kwamba nasema nimekuja kuwatumbua leo
lakini nina taarifa nyingi kuhusiana na rushwa inavyotembea katika ugawaji wa
vitalu’’
‘’Mtendaji
ifanyie kazi taarifa hii ya rushwa ila nikiona mambo hayaendi kama
ninavyotarajia nitakuja kivingine. alisisitiza
Katika
hatua nyingine , Naibu Waziri Hasunga ameiagiza TFS iongeze
ukusanyaji wa mapato kwa vile mapato yalipo sasa bado hayatoshelezi na
yaliyokusanywa yatumike vizuri.‘’Taarifa nilizonazo kuna maeneo manne mapato
yanavuja paangalieni hapo mparekebishe ‘’ alisema
Wakati
huo huo, Hasunga ameiagiza TFS ianze kuwekeza katika maeneo ambayo inaona
inaweza kuzalisha zaidi kwa mfano kwenye maporomoko ya Kalambo ili
iweze kuongeza mapato
‘’Yale
maporomoko ukikaa Zambia huwezi kuyaona vizuri ila ukikaa Tanzania unayaona
vizuri’ tumieni fursa hiyo baada ya miaka miwili ijayo kinaweza kikawa kituo
kikubwa cha utalii nchini.’’
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo amemhakikishia Naibu Waziri
Hasunga kuwa atatekeleza maagizo yake yote aliyoyatoa kwa maslahi mapana
ya TFS.
0 Comments