JAMHURI
YA MUUNGANO WA
TANZANIA
TAARIFA
KWA UMMA
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inakanusha tangazo linalosambaa katika Mitandao ya Kijamii
linalomhusisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan kuwa atashiriki zoezi la
kupanda miti kwenye Chuo Kikuu Cha Dodoma siku ya tarehe 1-1-2018. Ofisi ya
Makamu wa Rais inapenda kuujulisha umma kuwa tangazo hilo si la kweli na Makamu
wa Rais hana ratiba ya kupanda miti kwenye chuo hicho kwa tarehe iliyotajwa.
Ikumbukwe kuwa siku ya tarehe 15-12-2017
wakati wa hafla ya kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan alitangaza kampeni ya kupanda miti Dodoma ambayo itaratibiwa
na Ofisi yake .
Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzingatia
matangazo, taarifa na ratiba zitakazotolewa na Ofisi yake kuhusu programu ya
upandaji miti Dodoma.
Imetolewa
na:
Ofisi ya Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dodoma
30 Desemba,
2017.

0 Comments