Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
mamia ya wanachama wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kabla ya kufungua mkutano
huo Mkuu wa (CWT )katika ukumbi wa
Chimwaga mkoani Dodoma. Wanachama hao wa CWT walisimama na kushangilia mara baada ya ahadi ya Rais Dkt. Magufuli
kuwaahidi kuendelea kutatua kero zao mbalimbali.
Mamia
ya Wajumbe wa Chama cha Walimu(CWT) wakishangilia ndani ya ukumbi wa Chimwaga
wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
alipokuwa akijibu kero zao mbalimbali walizoziwasilisha.
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakiwa wameshikana mikono
wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kabla ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kuhutubia na kufungua mkutano huo wa CWT katika ukumbi wa Chimwaga mjini
Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa muda
wa CWT, Waziri wa Elimu Profesa Joyce
Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, pamoja na mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli wakiimba wimbo wa mshikamano pamoja na Wajumbe wote wa Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wajumbe wa CWT katika ukumbi wa
Chimwaga.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza
viongozi wa muda wa Chama cha Walimu Tanzania walipokuwa wakiwasilisha hoja zao
mbalimbali zinazo wakabili walimu nchini katika mkutano mkuu wa CWT uliofanyika
katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi
ya wajumbe wa Chama cha Walimu CWT mara baada ya kuwahutubia katika ukumbi wa
Chimwaga mjini Dodoma.
PICHA NA IKULU








0 Comments