Wakiwa makaburini hapo, Ramsey na Mama Kanumba walitumia muda mwingi kukumbatiana na kulia kwa huzuni jambo lililoteka na kuvuta hisia za watu wengi.
Mbali na tukio hilo, Ramsey alizidisha machungu kwa mama huyo baada ya kuanza kutamka maneno kama anazungumza na marehemu Kanumba ambapo alimueleza mambo yenye kuumiza.
“Steven, kwa mara ya mwisho tulizungumza sote tukiwa hai lakini leo nimesimama kando yako ukiwa umelala chini ya mchanga hujitambui, kwangu ni zaidi ya msiba na kwa kweli nimeshindwa kuhimili jambo hili, najua huko uliko unaumia sana hususan ukizingatia ukweli kwamba tasnia ya filamu za Kitanzania inakufa,” alisema Ramsey katika mazungumzo yale na Kanumba aliyoyatoa kwa hisia kali hali iliyomsababishia Mama Kanumba maumivu makali. mpekuzihuru.co



0 Comments