YAH: UCHAGUZI MKUU WA SHIMIWI
Shirikisho la Michezo ya Wizara na
Idara za Serikali (SHIMIWI) linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa
Uchaguzi wa Shirikisho tarehe 16 Desemba, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano
wa Hoteli ya Mount Uluguru Mkoani Morogoro. Kwa mujibu wa Sura ya III
Ibara ya 15 (2) ya Katiba ya SHIMIWI Wajumbe wa Mkutano huu ni wenyeviti
wa Vilabu, Makatibu wa Vilabu na mjumbe mmoja aliyechaguliwa na Klabu
kuwakilisha katika Mkutano Mkuu wa SHIMIWI.
Aidha, Sura ya VII Ibara ya 38.1 (i- viii) ya Katiba Mkutano huu utawachagua Viongozi wafuatao;
- Mwenyekiti 2. Makamu Mwenyekiti 3. Katibu Mkuu 4. Naibu Katibu Mkuu
- Mweka Hazina 6. Mweka Hazina Msaidizi 7. Wajumbe watano (5) wa Kamati ya Utendaji 8. Wajumbe wawili (2) wa viti maalum Wanawake.
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wenye mamlaka ya kusimamia Uchaguzi huu tayari wameshatangaza nafasi hizo.
Hivyo, nawaomba watumishi
tujitokeze kugombea nafasi hizo pia waajiri kuwawezesha viongozi
waliotajwa katika para ya kwanza hapo juu wahudhurie katika Mkutano huu.
Kiongozi atakayeshindwa kuhudhuria Mkutano anapaswa kuwasilisha taarifa
itakayoeleza sababu za kutohudhuria ili Mkutano utoe maamuzi na endapo
zitakuwa nje ya uwezo wa Mkutano zitafikishwa kwa Mlezi wa Shirikisho
ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma.
Shirikisho linasikitishwa na
taarifa zinazotolewa na baadhi ya Watumishi kuwa SHIMIWI imefutwa. Kwa
taarifa hii nawajulisha Watumishi wote wa Serikali kuwa SHIMIWI bado ipo
na inaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Tunawaomba viongozi
kuendelea kusimamia shughuli za Michezo katika maeneo yao ya Kazi ili
kulinda na kuimarisha afya za Watumishi.
Moshi Y. Makuka
KAIMU KATIBU MKUU – SHIMIWI
0754 – 763140 Imetolewa leo Tarehe 12 Desemba, 2017

0 Comments