Mwenyekiti wa Ukoo wa Patel, Harish Patel akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= fedha zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na ukoo wa Patel pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Ukoo wa Patel ukiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Mkurugezi Mtendaji wa Taasisis ya Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi akongea na waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi shilingi 22,500,000/= na Ukoo wa Patel , fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Picha na JKCI
..............
Na Mwandishi Wetu
17/12/2017 Ukoo wa Patel umekabidhi kiasi cha shilingi 22,500,000/= fedha ambazo zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji
wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Akikabidhi
fedha hizo leo Mwenyekiti wa Ukoo huo Harish Patel alisema watoto wengi
wanazaliwa na ugonjwa wa moyo na wengi wao hawana fedha za kulipia matibabu
wameona kwa kidogo walichokipata kisaidie kulipa gharama za matibabu ya wagonjwa
hao.
“Kila
wakati, kila mwaka kutokana na kipato
tunachokipata tumekuwa tukisaidia jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo elimu na afya na leo hii tumeona furaha zaidi
kusaidia watoto”, alisema.
Akipokea
fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi aliushukuru Ukoo wa Patel
kwa kuona umuhimu wa afya ya mtoto na kusaidia kulipia gharama za matibabu na
kuziomba Taasisi, Mashirika na watu binafsi wenye uwezo wajitokeza kulipia matibabu ya watoto.
Prof.
Janabi alimalizia kwa kusema kuwa watoto
wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo ni wengi
kati ya watoto milioni mbili wanaozaliwa asilimia moja (1%) wanazaliwa
na matatizo ya Moyo hivyo bado fedha zaidi zinahitajika kwa ajili ya matibabu.




0 Comments