Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
(katikati) alipofanya ziara kwenye machimbo yaliyopo Igurubi Wilayani Igunga.
Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Manonga lilipopo wilayani humo, Seif Gulamali.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia)
akitembelea maeneo ya Machimbo ya Dhahabu ya Igurubi, Wilayani Igunga.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
akitembelea maeneo ya Machimbo ya Dhahabu ya Igurubi, Wilayani Igunga.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
akitembelea maeneo ya Machimbo ya Dhahabu ya Igurubi, Wilayani Igunga.
................
Serikali
imewataka Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini wenye migogoro kukaa chini
kujadili na kuondoa tofauti zao ili kuwa na uchimbaji unaokusudiwa.
Naibu
Waziri wa Madini Stansalus Nyongo alitoa wito huo juzi alipofanya ziara kwenye
maeneo ya Machimbo ya Dhahabu kwenye Tarafa ya Igurubi Wilayani Igunga na
kujionea shughuli zilizokuwa zikiendelea na kuzungumza na wachimbaji.
Wachimbaji
hao wa Igurubi walimueleza Nyongo changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo
migogoro baina yao ambayo walisema inasababisha shughuli za uchimbaji kuzorota
na hivyo kuwakosesha kipato.
Walimuomba
Naibu waziri Nyongo kuingilia kati kukomesha migongano iliyopo baina yao ili
waendeleze maeneo hayo.
“Mheshimiwa
Waziri kama unavyotuona, tumekaa tu, hawa wamiliki wa haya machimbo wapo kwenye
migogoro na hivyo tumeagizwa kuacha kuendelea na shughuli yoyote hapa,” alisema
Alfred Mateo ambaye ni miongoni mwa wachimbaji waliomueleza Naibu Waziri
changamoto zinazowakabili.
Naibu
Waziri Nyongo aliwaagiza wenye machimbo hayo kukaa pamoja kutazama namna ya
kuondoa tofauti zao ili shughuli za uchimbaji kwenye maeneo hayo zifanyike ili
wao na wachimbaji wajipatie kipato na
wakati huohuo Serikali ikipata mapato yake kutokana na uchimbaji.
“Nyinyi
mnavyoendelea kuzozana na kusimamisha uchimbaji watu wengi waliopo hapa
wanaathirika, ninaona kuna wananchi wengi maeneo haya wamekuja kufanya kazi
lakini hawana kazi kwa sababu ya migogoro yenu,” alisema.
Aliiagiza
Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Tabora, kuhakikisha anaratibu mazungumzo baina ya
wachimbaji wenye migogoro na apatiwe taarifa ya makubaliano yatakayofikiwa.
Aidha,
Nyongo alizungumzia wananchi wanaohodhi maeneo mengi bila ya kuyafanyia kazi
ambapo alisema Tume ya Madini itakapoanza kazi, maeneo hayo yatatazamwa na
kugawiwa upya kwa wananchi wenye nia ya dhati ya kuwekeza kwenye shughuli za
uchimbaji.
Alisema
leseni nyingi zimekwisha muda wake ipo haja ya kurudisha leseni hizo kwa
Serikali ili izigawe upya kwa wananchi wenye uhitaji wa maeneo ya uchimbaji.
“Wapo
wajanja wachache wanamiliki leseni nyingi wakisubiri wawekezaji, hawa
tutawanyanganya ili wananchi wapate maeneo kwani hawaziendelezi,” alisema.
Alisema
lengo la Serikali ni kuhakikisha migodi inatoa ajira kwa wananchi mbalimbali
wakiwemo wa maeneo yenye migodi na kwamba kutoendeleza migodi hiyo
kunasababisha ajira nyingi kupotea hali ambayo alisema Serikali haiwezi
kuifumbia macho.
“Sisi
kama Serikali tunataka migodi itoe ajira, lakini kama leseni nyingi
zinashikiliwa bila kuendelezwa inamaana ajira lukuki zimepotea, hiyo
haikubaliki.
Alisema
mara Tume ya Madini itakavyoanza kazi, itashughulika na suala zima la leseni
kwahiyo aliwaasa wananchi wenye uhitaji wa maeneo ambayo hayajaendelezwa
kufanya subira ili wapatiwe maeneo.
Hata
hivyo alionya kuwa watakaopewa maeneo wahakikishe wanafuata sheria, kanuni na
taratibu za uchimbaji ili kuwa na uchimbaji wenye tija ikiwemo uepukaji wa
migogoro na ajali machimboni.




0 Comments