Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Bwana Omari Khamis Othman Akizungumza na
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kulia) na Ujumbe
aliofuatana nao alipomtembelea ofisini kwake, wakati akiendelea na ziara
ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2017. Mkuu huyo wa Mkoa
aliahidi kushughulikia kwa karibu ombi lilitolewa na Kamishna Sururu, la
kupatiwa Viwanja kwenye maeneo yaaliyotengwa na Serikali ili kujenga
Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi la Uhamiaji Mkoani humo.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akisikiliza maelezo yanayotolewa
na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Iddi A. Iddi wa Kituo cha Uhamiaji
Bandari ya Wete, kuhusu ukaguzi wa Watu wanaotumia Bandari hiyo, ambapo
vyombo vyake havijaruhusiwa kisheria kusafirisha abiria. Ilielezwa kuwa
hiyo ni changamoto kubwa katika Bandari hiyo kwani abiria wengi
wanaotumia Bandari hiyo hudai kuwa wanakwenda kwenye visiwa vya jirani
vya Fundo, Uvinje na Kokota, badala yake wakifika Bandari bubu zilizoko
kijiji cha Mtambwe wanabadili chombo kuelekea Visiwa vya Mombasa, Kenya.
Yalisemwa hayo wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe
20 – 21 Disemba, 2017.
Mkuu
wa Bandari ya Wete, Bwana Hassan Hamad Ali akimpokea na kumkaguza
maeneo mbali mbali ya Bandari hiyo Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari
M. Sururu (wa pili kushoto) na Maafisa Waandamizi wa Uhamiaji
aliombatana nao katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20
– 21 Disemba, 2017. Kamishna Sururu alimtaka Mkuu huyo kushughulikia
kwa karibu changamoto iliyopo ya baadhi ya vyombo vya Usafiri “Majahazi”
bandarini hapo kupakia abiria kinyume cha Sheria.
Mkaguzi
wa Uhamiaji, Omari Saidi Mohamed akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji
Zanzibar, Johari M. Sururu (katikati) na Maafisa Waandamizi wa Uhamiaji
Aliombatana nao Nyumba za Makaazi ya Askari wa Uhamiaji zilizoko mtaa wa
Mtemani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ziara ya
kikazi Mkoani humo tarehe 20 - 21 Disemba, 2017. Kutokana na uchakavu wa
nyumba hizo, Kamishna Sururu aliagiza nyumba hizo zifanyiwe ukarabati
haraka iwezekanavyo, huku akiahidi kwamba, Idara yake kwa kushirikiana
na Serikali
Sheha
wa Shehia ya Gando, Bw. Jafari Suleiman Said (wa pili kulia)
akizungumzia uwepo wa Bandari bubu ya Chokaani, Shehia ya Gando Wilaya
ya Wete inayotumiwa na baadhi ya watu kuingia na kutoka Visiwani humo
kwenda visiwa vya Mombasa, Kenya. Hayo yalielezwa kwa Kamishna wa
Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu wakati akiendelea na ziara yake ya
kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21 Disemba, 2017.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kulia) akiwa mbele ya
Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba
iliyofanyiwa ukarabati mkubwa na kujengwa uzio hivi karibuni, akifafanua
jambo kuhusu mkakati wa Idara wa kuboresha Majengo ya Ofisi na Makaazi
ya Askari wa Uhamiaji kwa Mikoa yote Unguja na Pemba. Huo ni muendelezo
wa ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2018.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kushoto) akipokea
salamu za Wananchi wa Shumba Mjini, akiwa katika ziara ya kikazi tarehe
20 Disemba 2017, akitembelea Bandari Bubu iliyopo Shumba Mjini, Wilaya
ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambayo ni maarufu kwa shughuli za
Uvuvi na Biashara.
Mkuu
wa Diko “Bandari Bubu” ya Shumba mjini Bwana Hussein Rashid Omar,
akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari M. Sururu wakati
alipofanya ziara ya kikazi Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba
tarehe 20 Disemba, 2017, baadhi ya Majahazi (hayapo pichani) yanayofanya
safari zake kupitia Bandari bubu hiyo. Huku wananchi waliowazunguka
wakisisitiza kuwa wao wanuafata Sheria na Taratibu zote za Nchi
wanapotoka ama kuingia nchini ikiwemo matumizi ya Pasipoti na kuiomba
Idara ya Uhamiaji kusukuma mbele juhudi za Serikali kurasimisha Bandari
hiyo
Sheha
wa Shehia ya Kiuyu Mbuyuni, Bw. Ali Hamad Sharifu (wa pili kulia)
akimueleza Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kushoto
kwake), jinsi wanavyoshirikiana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji kwa
kutoa taarifa zinazosaidia kuwadhibiti baadhi ya Watu wasio waaminifu
wanaojaribu kuingiza wageni bila ya kufuata Sheria na Taratibu za Idara
ya Uhamiaji Nchini. Yalielezwa hayo wakati Kamishna akiendelea na ziara
ya kikazi, Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21 Disemba, 2017.
Kamishna
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akiambatana na Maofisa
waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi ya bandari Bubu
za Kiuyu na Mbuyuni, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati
alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali, Mkoani humo tarehe 20 –
21 Disemba, 2017. Wilaya ya Micheweni ina Bandari Bubu zaidi ya 80
Zinazotumiwa kuvuka mpaka wa majini kuingia Visiwa vya jirani pamoja na
Shimoni, Mombasa, Kenya ambapo wakaazi wa maeneo hayo wana muingiliano
mkubwa katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
0 Comments