Mchezo huo uliokuwa mkali na wa aina yake uliohudhuriwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, aliyekuwa mgeni rasmi, ulishuhudiwa kipa wa Azam FC, Abalora, akifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo mikali ya URA na kupelekea kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mechi hiyo.
Zawadi ya Sure Boy
Ubingwa huo walioutwaa Azam FC, wameutoa zawadi kwa kiungo wa timu hiyo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, na hii ni baada ya kufiwa na Mama yake mzazi wiki iliyopita wakati akiwa na timu hiyo kwenye harakati za kuwania taji hilo.
Hadi Azam FC inatwaa ubingwa, imeweza kucheza jumla ya mechi sita, ikishinda mara tano na kupoteza mmoja huku ikiruhusu nyavu zake kuguswa mara moja tu, na hii ni walipofungwa bao 1-0 dhidi ya URA kabla ya kulipa kisasi kwenye mchezo huo wa fainali.
Kikosi hicho kinatarajia kuondoka visiwani Zanzibar, leo Jumapili saa 3 asubuhi kurejea jijini Dar es Salaam tayari kabisa kuanza maandalizi ya kuwakabili Majimaji ya Songea na Tanzania Prisons ya Mbeya, katika mechi zijazo mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) zitakazofanyika wiki ijayo.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa hivi:
Razak Abalora, Himid Mao (C), Bruce Kangwa, Agrey Moris, Yakubu Mohammed, Abdallah Kheri/Joseph Mahundi dk 59, Stephan Kingue, Frank Domayo/Iddi Kipagwile dk 58, Salmin Hoza, Bernard Arthur/Shaaban Idd dk 58, Yahya Zayd/Enock Atta dk 64.

0 Comments