Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya
Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo
akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo
leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari
31. (Picha na Ngailo Ndatta
Dereva wa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Athuman Ramadhani akishiriki katika
zoezi la upigaji chapa katika Mkoa wa Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa
knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na
Ngailo Ndatta)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya
Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye
skafu) akiongea na wafugaji kuhusu upigaji chapa mifugo
kwenye Kijiji cha
Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo
Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta)
.........
Na John Mapepele, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi
anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka Wakuu
Wote wa Idara katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba timu
zote zilizosambaa kote nchini ziwe zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo
saa kumi na mbili jioni ziwe zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili
akabidhi rasmi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua
zaidi baada
ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.
ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.
“Wakuu Wote wa Idara,Mhe Waziri anataka Timu za
Chapa zirudi Dodoma.Leo saa 12 jioni apate taarifa ya mwisho ya upigaji chapa.
Mkurugenzi wa Mipango ratibu timu ya kukamilisha taarifa ” alisisitiza Mashingo
kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa Idara.
Aidha amezitaka Halmashauri zote nchini
kuhakikisha wamemaliza zoezi la kupiga chapa mifugo yao yote katika muda
wa nyongeza uliotolewa na
Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.
Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.
Akizungumza katika siku za mwisho wakati
anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa zoezi la kupiga chapa katika Mkoa wa
Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika matatizo
ya kupiga chapa mifugo ambayo inatoka nje ya nchi ambapo amesema
wakibainika watachukuliwa hatua kali.
Aidha, Dkt. Mashingo amewataka wafugaji wote wasio
raia wa Tanzania
waliyoingia katika mikoa ya mipakani kuondoa mifugo yao mara moja kwa kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
waliyoingia katika mikoa ya mipakani kuondoa mifugo yao mara moja kwa kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Katika hatua nyingine Dkt. Mashingo ambaye pia ni
mtaalam bobezi katika eneo la malisho ya mifugo amesema kufanikiwa kwa zoezi la
kupiga chapa kutasaidia usimamizi wa Sekta ya Mifugo hapa nchini ambapo alisema
awali inakadiliwa
kwamba 30% ya malisho yote nchini yalikuwa yakitumiwa na mifugo toka nje
ya nchi.
kwamba 30% ya malisho yote nchini yalikuwa yakitumiwa na mifugo toka nje
ya nchi.
Ameutaka Uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania
(CCWT) kutopingana na Serikali badala yake kuongeza ushirikiano na
kuwaelimisha wenzao kufuga kisasa ili kuondoa migogoro baina ya wafugaji na
watumiaji wengine wa
ardhi.
ardhi.
Awali Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Luhaga Mpina wakati akihitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa
lililofanyika katika wilayani Itilima mkoani Simiyu, Desemba 31mwaka jana
aliongeza siku 30 kwa halmashauri zote nchini ili kukamilisha zoezi la kupigaji
chapa mifugo huku akiwavua nyadhifa maafisa wawili wa Wizara kwa kushindwa
kusimamia zoezi hilo kikamilifu na wengine wawili wakipewa onyo kali.
Alida kuwa licha ya
kuwepo kwa baadhi ya changamoto zilizosababisha zoezi hilo kufanyika kwa
asilimia 38.5 tu kwa nchi nzima baadhi
ya watendaji wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo
Halimashauri ambazo zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa majina ya watendaji wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.
ya watendaji wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo
Halimashauri ambazo zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa majina ya watendaji wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.
Siku kumi na tano baada ya muda wa nyongeza wa siku
thelathini, Mhe. Mpina alitoa tathmini mbele ya Waandishi wa Habari mjini Dodoma,
kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo ambapo Mpina
alisema hadi kufikia siku hiyo ya Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359
sawa na asilimia 59.3 ya lengo walishapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia
20 ya tathmini ya awali iliyofanywa Desemba 31 Mwaka jana .
Aidha alisema wafugaji wote nchini watakaoshindwa
kupiga
chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26.
chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26.



0 Comments