Random Posts

Kocha Claude Puel ataka Riyad Mahrez kufanya maamuzi

 Kocha wa Leicester City Claude Puel amesema anataka Riyad Mahrez kufanya maamuzi kuhusiana na mustakabali wake baada ya mchezaji huyo raia wa Algeria kufunga goli moja na kusaidia mengine mawili katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Huddersfield.

Mahrez, ambaye makataba wake unamalizika majira ya joto mwaka 2020, aliwekwa katika maombi ya kutaka kuhama Mei mwaka jana, lakini alibakia na Leicester baada ya dau la Roma la paundi milioni 27 kukataliwa.
   Riyad Mahrez akiwa amemzungusha kipa na kufunga goli la kwanza
 Mshambuliaji Islam Slimani akifunga akifunga goli la pili la Leicester City

Post a Comment

0 Comments