Na Hamza Temba-Dar es Salaam
..........
SERIKALI
kupitia wizara zake nne tofauti imedhamiria kukabiliana na changamoto
mbalimbali za utoaji wa huduma kwa wageni wanaiongia na kutoka nchini
kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere (JNIA)
jijijini Dar es Salaam.
Changamoto
hizo ni pamoja na msongamano na joto katika eneo la kuchukulia mizigo,
muda mrefu wa upatikanaji wa hati za kusafiria kwa wageni wanaoingia
nchini pamoja na changamoto ya ufinyu wa eneo la kusubiri huduma
uwanjani hapo.
Mawaziri
wa Wizara hizo ambao wamefanya ziara ya pamoja katika uwanja huo jana
na kukagua shughuli za utoaji huduma ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dk. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk.Mwigulu Nchemba,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dk.Susan Kolimba na Naibu Waziri wa Ujenzi
na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Akizungumza
uwanjani hapo, Dk. Kigwangalla alisema wamefikia hatua ya kukutana
mawaziri hao baada ya wageni hasa watalii wanaiongia nchini kulalamika
kuwa wanatumia muda mwingi kuhudumiwa katika eneo la uwanja huo kiasi
cha kuwapotezea muda.
Dk.Kigwangala
amesema kutokana na malalamiko hayo ya muda mrefu na mengine kadhaa
hatua mbalimbali zimechukuliwa tangu Agosti 8 mwaka 2017 manaibu waziri
wa wizara hizo nne walipofanya ziara uwanjani hapo kwa ajili ya kutafuta
ufumbuzi changamoto hizo na kwamba kukutana kwao jana ni muelendezo wa
kushughulikia kero hizo ambapo mafanikio yameanza kuonekana.
Dk.Kigwangala
amesema ipo haja ya kuweka mikakati ya kuboresha huduma katika viwanja
vya ndege nchini ukiwamo JNIA huku akisisitiza umuhimu wa watendaji na
watoa huduma katika nafasi mbalimbali kuwa wakarimu kwa wageni.
Amesema
ni vema hata Polisi walioko uwanjani hapo wakimkamata mgeni basi badala
ya kutumia nguvu wawe na ukarimu kwani ni muhimu kumdhibiti mgeni bila
kutumia nguvu ili ikibainika hana kosa aachiwe na asiwe na malalamiko ya
kunyanyaswa.
Dk.Kigwangala amesema kuna haja kwa wageni wanapokuja Tanzania wakirudi makwao wasimulie ukarimu na uzuri wa nchini yetu.
Ameongeza
anatamani kuona kuanzia uwanjani hapo hadi hotelini ambako mgeni
anakwenda anatumia muda mchache, anapata nafasi ya kuona picha za
viongozi mbalimbali ambazo zitakuwa uwanjani, picha za wanyama na video
ambazo zinaonesha utalii wa Tanzania.
Amesema
kumpokea mgeni jambo moja lakini namna ya kumhudumia ni jambo jingine
na ndilo muhimu zaidi na akafafanua hata teksi ambayo mgeni ataitumia
kusafiri dereva awe na ukarimu hata wa kumsalimia na wakati mwingine
kutabasamu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Mambo ya ndani Ndani Dk. Mwigulu Nchemba
akizungumza baada ya ziara hiyo alisema jitihada mbalimbali zinafanywa
kutatua changamoto hizo.
Ametaja hatua ambazo wizara yake inachukua ni kuharakisha utoaji huduma wa hati za kusafiria kwa njia ya kieletroniki.
Pia
wameamua kuongeza idadi ya madawati ya kutolea huduma kwa wageni ikiwa
sambamba na kuongeza watoaji huduma ili kurahisisha utoaji huduma wa
muda mfupi.
“Taarifa
zinaonesha kuwa kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa kutoa huduma kwani
badala ya saa tatu ambazo zilikuwa zinatumia awali hivi sasa muda wa
utoaji huduma umeshuka hadi saa moja, lengo letu ni kushuka zaidi.
“Mbali
ya kuboresha huduma tutahakikisha pia tunaongeza ulinzi na usalama
katika viwanja vyetu vyote nchini ili kudhibiti wageni wenye nia ovu na
nchi yetu.
“Tunafahamu
mataifa mengi yameitikia mwito wa uwekezaji nchini hasa katika mikakati
ya kufikia Serikali ya Viwanda na uchumi wa kati.
“Hivyo
wageni wanakuja kwa nia njema ya kuwekeza lakini hatutaki wale wenye
nia mbaya kutumia mwanya huo.Hivyo tutaendelea kuimarisha ulinzi na
usalama katika viwanja vyetu,”amesema.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk.
Susan Kolimba amesema wanaridhishwa na hatua ambazo zinachukuliwa
katika kuondoa changamoto zinazoelezwa kuwapo uwanjani hapo.
Amesema
wizara yao inatamani kuona idadi ya wageni inaongezeka zaidi na wakati
huo huo wakifurahia huduma ambazo wanazipata wakifika nchini kwetu.
Alisema Wizara yake itaendelea kuitangaza Tanzania na vitutio vyake ili
idadi ya watalii iweze kuongezeka.
“Tumefanya
ziara na binafsi niseme tu nimeridhishwa na hatua ambazo zinachukuliwa
katika kuondoa changamoto hizo,”amesema Dk.Kolimba.
Naye,
Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye
amesema wizara yao tayari imechukua hatua mbalimbali za kuondoa
changamoto zilizopo ikiwamo ya kufunga viyoyozi (AC) kwa ajili ya
kuondoa hali ya joto.
“AC
zilizopo ni za muda mrefu kwani ziliwekwa tangu majengo ya uwanja huo
yalipojengwa. Hivyo tayari zimeanza kufungwa AC mpya na ndio maana joto
limepungua” amesema.
Pia
amesema wamepata kampuni ambayo itakayofanya ukarabati kwa kuongeza
eneo la kukaa wageni wanaosubiri huduma mbalimbali kabla ya kutoka
uwanjani.
Amesema
kuna jitihada mbalimbali Serikali inafanya jitihada za kuondoa
msongamano wa wageni ikiwamo ya kuharakisha ujenzi wa jengo jipya la
kusafiria wageni la Terminal III ambalo litahudumia watu milioni sita
badala ya jengo la sasa ambalo wakati linajengwa lengo lake lilikuwa
kuhudumia watu milioni moja.
“Ujenzi
wa jengo jipya umekamilika kwa asilimia 70 na litakapokuwa tayari kwa
asilimia 100 litaanza kutumika kwa kuwa kasi ya ujenzi inakwenda
vizuri,’amesema.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba wakati wa ziara ya pamoja
ya kukagua Changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wageni hususan
watalii wanaoingia nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam JNIA jana kwa ajili ya kukabiliana nazo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es salaam jana wakati wa ziara ya pamoja ya
kukagua Changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wageni hususan watalii
wanaoingia nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam
JNIA kwa ajili ya kukabiliana nazo. Wengine walioshiriki ziara hiyo ni
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba (wa pili kulia), Naibu
Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu
kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Dk. Susan Kolimba (wa nne kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Susan Kolimba jijini
Dar es salaam jana wakati wa ziara ya pamoja ya kukagua Changamoto
mbalimbali wanazokumbana nazo wageni hususan watalii wanaoingia nchini
kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam JNIA kwa ajili ya
kukabiliana nazo. Wengine walioshiriki ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya
Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba (wa tatu kushoto) na Naibu Waziri wa Ujenzi
na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) .
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Susan Kolimba jijini
Dar es salaam jana wakati wa ziara ya pamoja ya kukagua Changamoto
mbalimbali wanazokumbana nazo wageni hususan watalii wanaoingia nchini
kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam JNIA kwa ajili ya
kukabiliana nazo. Wengine walioshiriki ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya
Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba (kulia) na Naibu Waziri wa Ujenzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia).
Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dkt. Susan Kolimba kulia akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba kushoto, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi
Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) na Waziri wa Maliasili na Utalii
Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) wakati wa ziara hiyo.
0 Comments