Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Muongozo wa
Matibabu na Orodha ya dawa muhimu wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini
Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali prof. Mohammed
Bakari Kambi na kushoto ni Mwakilishi wa WHO.
PICHA NA WIZARA YA AFYA.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto mwenye kilemba akiwakabidhi baadhi ya
wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Afya nchini Muongozo wa Matibabu na orodha
ya dawa wakati wa uzinduzi wa Muongozo huo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kushoto akionyesha Muongozo wa Matibabu na
orodha ya dawa zote muhimu wakati wa uzinduzi wa Muongozo huo jijini Dar es
salaam, wa kwanza kuhoto ni Mganga Mkuu wa Serikali prof. Mohammed Bakari Kambi
,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kinga na Ubora Wizara ya Afya Dkt. Mohammed
Mohammed na anayefuata ni mwakilishi wa WHO.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo
pichani wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote
muhimu jijini Dar es salaam.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya imeandaa Muongozo wa matibabu nchini na orodha ya dawa
zote muhimu ili kuepukana na tatizo la usugu wa vimelea vya dawa.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote
muhimu uliofanyika jijini Dar es salaam.
"Ni
muhimu kila kituo cha afya kuwa na dawa za kutosha, vifaa na vifaa tiba lakini
ni lazima tuzingatie muongozo wa matibabu na orodha ya dawa kulingana na
ugonjwa fulani ili kuepuka tatizo hili" alisema Waziri Ummy
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa Muongozo huo umezingatia vigezo vyote vya kuweka dawa
ambazo zilikuwa hazipo katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya
ambazo zimepata uthibitisho kutoka Shirika la Afya la Dunia (WHO).
Aidha
Waziri Ummy amewapiga marufuku Bohari Kuu ya dawa ya Taifa MSD na Mfuko wa Bima
ya Afya wa Taifa (NHIF) kuagiza na kuandika dawa zilizo nje ya muongozo
uliozinduliwa leo ili kuondoa matumizi ya dawa yasiyo sahihi.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kila kituo cha afya ni lazima kiongozwe na
Tabibu na sio vinginevyo ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana katika
kituo cha afya husika.
Kwa
mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa itafika kipindi vituo vya afya ambavyo
havikizi vigezo vitafungiwa ili kuepuka usababishwaji wa vifo visivyo vya
lazima kwa watanzania.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi amesema kuwa
muongozo wa kutibu magonjwa mbambali
umezingatia
Orodha ya dawa ambazo zitakuwa zinatumika nchini kwetu kama dawa muhimu za
kutibu magonjwa hayo.






0 Comments