Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimjulia hali mgonjwa aliyelazwa kwenye
hospitali ya taaluma na Tiba Mloganzila wakati alipotyembelera hospitali hiyo
ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wananchi waliokuwa wanasuburi
huduma kwenye hospitali ya taaluma na Tiba Mloganzila wakati alipotyembelera
hospitali hiyo ili kuangalia hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam..
wa kwanza kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali hiyo
Prof. Aboud Said.
Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na waandishi wa habari
alipotyembelea hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila ili kuangalia hali ya
utoaji huduma leo jijini Dar es salaam,wa kwanza kushoto ni Naibu Makamu Mkuu
wa Chuo na Huduma za Hospitali hiyo prof. Aboud Said.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Huduma za Hospitali
Mloganzila wa kwanza kulia Prof. Aboud Said. Akizungumza na waandishi wa habari
wakati Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu katikati alipotyembelea hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila ili kuangalia
hali ya utoaji huduma leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikatiakitembelea maeneo ya Hospitali ya Taaluma na
Tiba Mloganzila alipotyembelera hospitali hiyo ili kuangalia hali ya utoaji
huduma leo jijini Dar es salaam.. wa kwanza kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa
Chuo na Huduma za Hospitali hiyo Prof. Aboud Said.
Picha na Ally Daud-Wizara ya Afya
...........................
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb) leo
Januari 10, 2018 ametembelea Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo cha Afya na
Sayansi Shirikishi Cha Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila iliyofunguliwa
rasmi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Novemba 25, 2017.
Lengo la kutembelea hospitali hiyo ni kuangalia utoaji wa
huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hiyo.
Baada ya
kutembelea hospitali hiyo Waziri Ummy ameagiza Idara yote ya magonjwa ya ndani
(Internal Medicine) iliyopo hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhamia mara moja
katika hospitali hiyo wakiwemo Madaktari ,Madaktari Bingwa, Wauguzi pamoja na
wataalamu wengine wa idara hiyo.
Wakati
huo huo Waziri Ummy ameagiza kuhamisha wagonjwa waliopo wodi namba 3, 4,5,6,7
na 8 zilizopo kwenye jengo la Mwaisela Muhimbili na kupelekwa hospitali ya
Mloganzila isipokuwa wagonjwa walio mahututi na wenye sababu maalumu na baada
ya kuondoka wagonjwa hao wodi hizo zifanyiwe ukarabati mara moja.
”Nawaagiza
waganga wafawidhi wa hospitali za Rufaa za Temeke,Mwananyamala na Amana kuanzia
sasa rufaa zote za wagonjwa wa magonjwa ya ndani zije Mlongazila”, Aliongeza
Mhe. Ummy.
Aidha,
Waziri Ummy alisema Wizara imeshapokea Hospitali za Rufaa za Mikoa kutoka
TAMISEMI hivyo amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara hiyo kukamilisha kuwapangia
baadhi ya Madaktari Bingwa waliopo hospitali hiyo ya Taifa na kuwapeleka
hospitali za Rufaa za Mkoa na Kanda mapema Februari mwaka huu.
“Tumeomba kibali
Utumishi wa Umma ili kuwahamisha Madaktari Bingwa zaidi ya ishirini (20)
waliopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) pamoja na mishahara
yao,”Madaktari wetu ni Wazalendo wapo tayari kwenda kutoa huduma za matibabu ya
kibingwa kwenye hospitali zetu za Mikoa na Kanda”.
Alisema
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuwahudumia wananchi wote
ikiwemo kupata huduma za matibabu ya kibingwa bila kubagua hivyo Wizara yake
imejipanga kununua vifaa na vifaa tiba na kuvisambaza kwenye hospitali hizo za
rufaa za Mikoa.
Alitaja Madaktari Bingwa watakaohamishiwa kwenye Hospitali za
Rufaa za Mikoa na Kanda miongoni mwao ni wa Magonjwa ya akina Mama na
Uzazi, Watoto, Upasuaji wa jumla, Radiolojia, Usingizi Macho pamoja na
Magonjwa ya ndani.
Mloganzila
ni Hospitali ya Taaluma na Tiba ambayo imewekwa
vifaa tiba vya kisasa na teknolojia ya hali ya juu na ina vitanda
571 vya kulaza wagonjwa na vyumaba 13 vya upasuaji na inatoa huduma masaa
ishirini na nne.
Imetolewa
na
Catherine Sungura
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Afya
10/1/2018





0 Comments