Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 192 wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania pamoja na Maafisa kadhaa kutoka nchi marafiki katika
Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakivalishana vyeo mara baada ya
Kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi wakila Kiapo cha Utii kwa Amiri Jeshi
Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika
viwanja vya Ikulu mara baada ya kutunukiwa Kamisheni.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akikagua gwaride la Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na
baadhi kutoka nchi marafiki kabla ya kuwatunuku Kamisheni katika viwanja vya
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha
Monduli (TMA) Meja Jenerali Paul Peter Masao katika picha ya pamoja na
Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi pamoja na baadhi kutoka nchi marafiki mara
baada ya kuwatunuku Kamisheni.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati Bendi ya Jeshi la Ulinzi ilipokuwa ikitoa
burudani katika viwanja vya Ikulu mara baada ya kuisha kwa shughuli za Kutunuku
Kamisheni.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akielekea kutunuku Kamisheni katika Viwanja vya Ikulu.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa maafisa
wapya wapatao 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi pamoja na baadhi kutoka nchi
marafiki.
PICHA NA IKULU

0 Comments