Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na
Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye
pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na
kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo
Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi
huo wakati wa utekelezaji.
Miongoni
mwa mambo waliyojadili ni kuboresha miundombinu ya barabara kuunganisha
maeneo ya vivutio na miji ya ukanda huo pamoja na viwanja vya ndege
ndani ya hifadhi viwe na hadhi na ubora wa kutua ndege kubwa ikiwemo za
Air Tanzania.
"Nawapongeza
kwa mradi huu ambao ni mzuri sana kwenye uhifadhi lakini una mapungufu
kidogo kwenye biashara ya utalii jambo ambalo ni muhimu kuangaliwa ili
uwe na tija zaidi kwa jamii na taifa kwa ujumla" alisema Dk.
Kigwangalla.
Alimuomba
mratibu huyo kuona namna ya kubadilisha vipengele vya utekelezaji wa
mradi huo ili uweze kuwa na tija zaidi hususan suala la miundombinu ya
kuunganisha hifadhi mbalimbali za ukanda huo na miji ili kurahisisha
usafiri wa kufikia vivutio hivyo kwa muda mfupi na kwa wakati.
Kwa
upande wake mratibu huyo alisema jambo hilo linajadilika na kwamba
uendelezaji wa maeneo hayo ni mtambuka ukihusisha Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi ambazo nazo zimeahidi kuboresha miundombinu ya maeneo hayo.
Mradi
wa REGROW unatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12 Februari mwaka huu
Mjini Iringa na Mhe. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Mwezi Agosti
mwaka jana Serikali ya Tanzania ilisaini mkopo wa masharti nafuu wa Dola
za Kimarekani Milioni 150 sawa na takriban bilioni 340 za Tanzania kwa
ajili ya kuendeleza mradi huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisisitiza
jambo wakati wa mazungumzo na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini
Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW
kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa
Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili
mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. Kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza
Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye
pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na
kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo
Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi
huo wakati wa utekelezaji.
(PICHA NA HAMZA TEMBA-WMU)
No comments:
Post a Comment