Dk. Mwigulu Aongoza Operesheni Mashamba ya Bhangi Yaliyopo Mafichoni - MTAZAMO MEDIA

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 7 February 2018

Dk. Mwigulu Aongoza Operesheni Mashamba ya Bhangi Yaliyopo Mafichoni

 KAZI NA DAWA, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba akihamasisha askari kuimba nyimbo mbalimbali za uzalendo wakati wa operesheni ya kuharibu mashamba ya bhangi iliyofanyika wilayani Arumeru, nyuma yake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (DCP) Charles Mkumbo. 
(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba akiwa pamoja na Kamanda wa Polisi wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu kamishna (DCP) Charles Mkumbo wakati wa operesheni ya kuharibu mashamba ya bhangi iliyofanyika jana kwenye mashamba yaliyopo katika kijiji cha Engalaoni Kata ya Musa wilaya ya Arumeru.
 (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba akishuka kwenye moja ya mteremko mkali kuelekea kwenye mashamba ya bhangi yaliyopo mafichoni katika kijiji cha Engalaoni kata ya Musa wilayani Arumeru. 
(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba jana aliongoza operesheni ya kuharibu mashamba ya bhangi yaliyopo mafichoni iliyofanyika katika kijiji cha Engalaoni kata ya Musa tarafa ya Muklati wilayani Arumeru.

 Akizungumza katika mashamba hayo ambayo yamelimwa nyuma ya milima ambayo yapo umbali mrefu na makazi ya watu, Dr. Mwigulu alitoa tahadhari kwa wananchi wanaojihusisha na kilimo hicho huku akisisitiza serikali itaendelea kupambana nao na kuwafikisha Mahakamani.

“Natoa tahadhari kwa wananchi wote wanaolima zao hilo ambalo halikubaliki kwamba, vita hii ni vita endelevu na wamiliki watafikishwa Mahakamani”. Alionya Dr. Mwigulu na kushauri kwamba wanachi wanatakiwa kubadilika na kulima mazao mbadala ambayo yanakubalika kama vile Pareto, Viazi mviringo, na Karoti.

Alisema wale wote ambao wanaendelea kutoa  vyombo vyao vya usafiri kwa ajili ya kusafirisha zao hilo haramu wajue wanatenda kosa na wakikamatwa vyombo vyao vitataifishwa.

Dr. Mwigulu alimtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha aendelee kusonga mbele na timu yake huku akimpongeza kutokana na operesheni za mafanikio alizozifanya hasa za matumizi ya silaha na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Akizungumza katika Operesheni hiyo  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna  (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba, zoezi la kutafuta mashamba ya bhangi yaliyopo kwenye maficho ni endelevu.

Alisema wananchi wanatakiwa waachane na kilimo cha zao hilo kwani Jeshi la Polisi lina mtandao mkubwa wa kubaini uhalifu kwani popote watakapolima watagundulika  na kuongeza kwamba, wakulima wa zao hilo wataendelea kuteseka kwa kukimbia kimbia lakini mwisho wa siku watakamatwa na sheria kuchukua mkondo wake.

Akizungumzia juu ya tahtmini ya uelekeo wa mafanikio ya Operesheni hizo hasa katika wilaya ya Arumeru, Kamanda Mkumbo alisema kwa sasa udhibiti umekuwa mkubwa tofauti na awali ambao unasababisha wahalifu hao kukimbilia mafichoni badala ya mashamba yaliyo katika maeneo ya wazi na kusisitiza kwamba, Jeshi hilo litaendelea kubandika mguu pale ambapo wao watakuwa wananza kulima.

Jumla ya hekari zilizokadiriwa sita ziliharibiwa kwa kufyekwa ambapo vikosi vya Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo mkoani hapa pamoja na wilaya ya Arumeru viliungana na kufanikisha kazi hizo baada ya kupanda milima mirefu kwa muda wa saa mbili kutoka walipoacha magari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages