Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya siku nne mkoani Iringa ikiwa na lengo la
kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo na kuzindua mradi wa kuendeleza
utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania – REGROW.
Mara baada ya kuwasili mkoani Iringa , Makamu wa Rais
alifungua wodi mpya katika Zahanati ya Kising’a ambapo aliwaomba wananchi wote
wajiunge na mfuko wa bima ya Afya ili waweze kunufaika na huduma bora za afya.
“niwaombe sana ndugu
zangu kila mmoja ahakikishe ana bima ya afya, bima ya afya ndio mkombozi wako,
unapopata mavuno yako weka pesa ya bima ya afya”
Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Wananchi hao kwa mwamko wa
kuchangia ujenzi na kutoa eneo lakini pia pongezi kwa umoja wa makampuni ya
Asas kwa ufadhili wa shilingi za kitanzania milioni 125.
Makamu wa Rais alisema Ilani ya CCM inatuagiza kujenga
zahanati katika kila kijiji hivyo ujenzi wa Wodi hii katika Zahanati ya Kising’a
ni utekelezaji wa maagizo ya Ilani hiyo.
Makamu wa Rais aliwataka wananchi kuendelea kuchukua
tahadhari dhidi ya ugonjwa wa ukimwi kwani unapoteza nguvu kazi ya Taifa kwani mpaka sasa wastani wa
maambukizo umeongezeka mpaka kufikia asiliamia 22.3 kwa mwaka 2016/17 toka
asilimia 9.1 mwaka 2011/ 2012.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitembelea kiwanda cha Ivori Food &
Bevarage na kujionea namna kiwanda hicho
kinavyozalisha bidhaa zake kwa kutumia malighafi kutoka ndani ya nchi ikiwemo
Cocoa toka Kyela,Nyanya toka Ilula, mahindi toka kwa wakulima wa Iringa, Rukwa
na Ruvuma.
Aidha Makamu wa Rais alitembelea kampuni ya GBRI Business Solutions
inayozalisha bidhaa za mboga mboga za EatFresh na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo Bi. Hadija Jabir
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi waliojitokeza wakati
wa ufunguzi wa wodi katika zahanati ya Kising’a mkoani Iringa.
(Picha na Ofisi
ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya Wakazi waliojitokeza wakati wa
ufunguzi wa wodi katika zahanati ya Kising’a mkoani Iringa ambapo Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa mgeni Rasmi.
(Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.
Amina Masenza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kising’a tayari kwa ufunguzi wa wodi katika Zahanati
ya Kising’a.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya uendeshaji na
uzalishaji wa kiwanda cha Ivori Food & Bevarage cha Iringa kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji Bw. Suhail Esmail Thakore.
(Picha na ofisi
ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
wafanyakazi wa kampuni ya GBRI inayozalisha bidhaa za mboga mboga
zinazojulikana kama Eat Fresh mjini Iringa.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa baadhi ya
bidhaa za mboga mboga za Eat Fresh na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GBRI
Bi. Hadija Jabir.
No comments:
Post a Comment