Makamuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassa amewataka
Viongozi wa mkoa na wilaya mkoani Simiyu kusimamia sheria na kutowafumbia macho
wanaowapa mimba wanafunzi.
Akizungumza
na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwandoya
Kisesa, wilayani Meatu.
Makamu
wa Rais alisema “Jamani mnadhulumu
watoto wetu hapa kuna kina Samia wa baadae mnapokuja kuwapa ujauzito mapema
mkawavunjia safari zao, mkawaoa mapema, wakina Samia hawataibuka Meatu,
tutatoka huko nje tutaibuka hapa Meatu, tunataka Samia atoke hapa Meatu
waachieni wasome, masuala ya mimba za utotoni wapunguzieni.”
Makamu
wa Rais aliwahimiza wananchi kujiandikisha kwa wingi kwenye mifuko ya bima ya
afya kwani inafaida kubwa sana.
“Magonjwa yaweza kukufika wakati huna
pesa na kitu pekee kitakachokusaidia ni bima yako ya afya hivyo wananchi
hakikisheni mnapovuna na kuuza mazao yenu mnapata bima ya afya”
Makamu
wa Rais aliwapongeza wananchi wa Wilaya ya Meatu kwa kulima pamba kwa wingi
ambapo wilaya hiyo inategemea kilo 84 na kuwaahidi wananchi hao kuwa dawa za
kuulia wadudu zitapatikana kwa wingi kuanzia mwisho wa mwezi huu kwani serikali
imetoa fedha zaidi ya bilioni 9 .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Mwandoya jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa barabara zote ambazo ilani ya uchaguzi imeahidi
kuzijenga zitajengwa na zile ambazo hazipo kwenye ilani ila zina umuhimu
zitaingizwa kwenye bajeti ijayo.
Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Kisesa
Mhe. Luaga Mpina alisema kuwa kati ya kata 13 ni vijiji vine tu vina maji hivyo
alimuomba Waziri wa Maji kusaidia zaidi upatikanaji wa maji.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe aliahidi kusimamia kwa
ukamilifu upatikanaji wa maji .


0 Comments