Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili
Jijini Mwanza Februari 18, 2018 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony
Mtaka.
Makamu wa
Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kesho
mkoani Simiyu.
Katika ziara
hiyo itakayoanza kesho tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe 22/2/2018, Makamu
wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi
wa maji Kiloleli na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza
na wanachi Lamadi .
Pia Makamu
wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa
mkoa katika eneo la Nyaumata.
Miradi
mingine ambayo Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za
Lami Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za
Mjini.
Makamu wa
Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi
siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya (Meatu)
Tarehe 21,
Makamu wa Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda
Tanzania kasha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya Itilima na
kusalimia wananchi, kufungua jingo la upasuaji
la Samia Suluhu Hassan katika
Hospitali ya Wilaya ya Maswa na
kuzungumza na wananchi katika viwanja vya nguzo nane.
Siku ya
tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali
ya 34 ya Chuo Kikuu Huria .



0 Comments