Mbunge
wa Lupa Mhe. Victor Mwambalaswa akiwasisitiza wabunge wenzake umuhimu wa kupima
afya zao hasa tezi dume kwa wanaume wakati wa semina ya afya ya moyo na
magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa
Pius Msekwa mjini Dodoma.
Mbunge wa Bunda mjini Mhe. Ester Bulaya akieleza jinsi anavyoridhishwa na huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na JKCI ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea mpango wa Serikali kupitia Hospitali za mikoa wa kusomesha madaktari bingwa wengi ili kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalam hao wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Daktari wa Bunge Jeminian Temba mara baada ya kumalizika kwa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma. Katikati ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Yona Gandye.

Wabunge wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) akielezea kuhusu
dalili za shinikizo la damu na tiba yake wakati wa semina ya afya ya moyo na magonjwa
yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo
ilifanyika jana katika ukumbi wa Pius
Msekwa mjini Dodoma.
Picha na JKCI
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Wazazi
wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo zote zinazotakiwa ili
waweze kuepukana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo ya kuzaliwa
nayo.
Rai hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiongea na wabunge
waliohudhuria semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa
na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Waziri Ummy aliwaomba wabunge hao kila wanapokutana na
wananchi kupitia mikutano ya hadhara wawasisitize umuhimu wa kuwapeleka watoto wao
katika vituo cha afya ili wakapate chanjo zinazohitajika kwa wakati.
Aidha Waziri huyo alisema kuwa matibabu ya moyo pamoja na magonjwa mengine
yasiyoambukiza ni ya gharama kubwa na kuwaomba wabunge hao kuwahimiza wananchi
kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao utawasaidia kupata matibabu
katika Hospitali zote nchini ikiwemo
JKCI na Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika hatua nyingine Mhe. Ummy aliwataka wakurugenzi wa
Taasisi zingine kuiga mfano wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete Prof. Mohamed ambaye kupitia uongozi wake na jitihada zake binafsi
Taasisi hiyo imeweza kutoa huduma bora na kuwahudumia wananchi vizuri katika matibabu ya moyo na hivyo kuokoa maisha ya
watanzania wengi.
“Katika utendaji kazi wa Taasisi hii tunaona juhudi binafsi za
kiongozi ambaye kwa jitihada zake
amewatumia marafiki aliosoma nao
na kufanya nao kazi katika nchi mbalimbali kuja nchini kutoa mafunzo kwa
wataalam wetu na huduma za matibabu magumu ya moyo ambayo sisi peke yetu tusingeweza
kuyafanya kutokana na uchanga tulionao”, alisema Waziri Ummy .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo
ya Jamii Mhe. Peter Serukamba aliomba katika kikao cha Bunge la Bajeti wabunge wapewe
semina kama hiyo ambayo itaenda sambamba
na upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo, saratani za matiti na shingo ya kizazi, tezi
dume na kisukari.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi
aliwasisitiza wabunge kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara
ili kama watakutwa na matatizo waweze kupata matibabu kwa wakati, kufanya
mazoezi na kuepuka kula vyakula ambavyo vitawaepusha kupata magonjwa ya moyo na
mishipa ya damu.
Katika semina hiyo ya siku moja mada mbalimbali zilijadiliwa
ikiwa ni pamoja na Shinikizo la damu na
dalili zake na tiba , kiharusi, tezi dume na wanawake kukoma kwa hedhi kwa wanawake.
No comments:
Post a Comment