Random Posts

The Mafik laja kuwashika

Mtazamo News--

KUNDI la The Mafik linaloimba muziki wa aina mbalimbali limezinduliwa juzi usiku huku wasanii watatu wanaounda kundi hilo wakiahidi kuleta mabadiliko katika tasnia ya muziki hapa nchini hasa muziki wa kundi

Wasanii wanaounda kundi hilo ni Rhino, Hamadai na Mbalamwezi ambao wote ni wasanii wa muziki wa dansi pia kwa kuwa wametokea kwenye bendi ya The Mafik Band inayopiga kila Jumapili klabu ya Next Door Oyster bay, Dar es Salaam.

Akizungumzia ujio wa kundi hilo, Meneja wa kundi, Michael Mlingwa (Mx Carter) aliweka wazi kuwa kundi hilo hadi sasa lina nyimbo tano ambazo pia video zake zimerekodiwa nchini Afrika Kusini.

Alisema, kwa hiyo juzi wametambulisha wimbo wao mmoja uitwao Passenger ambao unaingia rasmi sokoni leo huku ukiwa ummeshatengenezewa video yake pia.

Alisema, wasanii wa kundi hilo wanaweza kuimba kila aina ya wimbo kwa kuwa ni wasanii ambao wamekulia kwenye muziki na wamekuwa wakifanya muziki hasa wa bendi kwa muda mrefu.

Alisema" vijana hawa watakuwa wakifanya kazi kama wasanii watatu kwa pamoja na watakuwa wakiimba muziki wa kawaida na hata kwa bendi inategemea na uhitaji wa mteja lakini ni wasanii ambao wamekuja kufanya makubwa kwenye fani hii".

Majina ya wasanii wa kundi hilo ni Salehe Hussein( Rhino King) Mohamed Mkumba( Hamadai) na Abdallah Yusuph (Mbalamwezi) ambapo Mbalamwezi aliwaambia wapenzi wa muziki nchini kutarajia kupata burudani safi ya muziki.

"Hili ni kundi jipya lakini kwa maana ya tunaoliunda ni wanamuziki wa muda mrefu kwenye medani hii ya muziki hapa nchini, tumekuwa kwenye bendi na kwa sasa tunasimama kama wasanii wa kundi ambao pia tupo kwenye bendi"
  Kundi jipya la muziki liitwalo The Mafik Band. 
 Meneja wa msanii wa muziki Shetta, Mx Carter akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa Kundi jipya la muziki liitwalo The Mafik Band' uliofanyika katika Club Next Door Masaki Dar es salaam .
 Shetta akizungumza.
 Msanii wa kundi la The Mafiq, Salehe Hussein (Rhino King) akiimba kwenye uzinduzi wa kundi hilo jana kwenye klabu Next Door kulia kwake ni Mohamed Mkumba( Hamadai) wakati kulia ni Abdallah Yusuph (Mbalamwezi)
Wadau wakishuudia uzinduzi huo.

Post a Comment

0 Comments