Picha na Tiganya Vincent
Baadhi ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 4.4 vilivyotolewa jana na Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania Ltd kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Mkoa wa Tabora za kampeni yake ya kuhakikisha eneo hilo linakuwa la kijani kwa kupanda miti kwa wingi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya thamani ya milioni 4.4 ambavyo vitasaidia katika kampeni ya uhifadhi mazingira na upandaji miti . Vifaa hivyo vimekabidhiwa jana na Kampuni ya Alliance One Tobacco Tanzania Ltd.
NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA
KAMPUNI ya Alliance One Tobacco Tanzania Ltd imeukabidhi Mkoa wa Tabora vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya upandaji miti na uhifadhi wa mazingira katika maeneo mbalimbali zinasimamiwa na viongozi wake.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 4.4 vimekabidhiwa jana na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa zao hilo wa Kampuni hiyo David Mayunga kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.
Alisema kuwa wakiwa wanunuzi wa tumbaku wameamua kukabidhi vifaa hivyo ili kuunga mkono jitihada za upandaji miti katika maeneo mbalimbali ikiwemo Vyama vya Ushirika vya Msingi zinasimamiwa na Mkuu wa Mkoa za kuhakikisha kuwa miti inapandwa na mazingira yanatunzwa.
Mayunga alisema kuwa Mkuu wa Mkoa ameonyesha jitihada kubwa za kuhakikisha miti inapandwa kwa wingi na hivyo wameamua kutoka vifaa kama vile majembe(20), nyundo (10), Kamba (10) na Keni za kumwagilia maji(Watering Can) (20) ili kuunga mkono jitihada hizo.
Alisema kama Kampuni inahusika na ununuzi wa zao tumbaku ambalo kwa kiasi kikubwa linategemea nishati inayozalishwa na kuni wakati wa ukaushaji wake wanaendelea kuunga mkono juhudi za kupanda miti katika mashamba mbalimbali yao na katika vyama vya msingi na wadau wengine ili kuhakikisha mazingira yanakuwa endelevu.
Akipokea vifaa hivyo , Mkuu wa Mkoa aliishukuru Kampuni ya Alliance One kwa msaada huo na kusema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kukabiliana na upungufu wa vitendea kazi pindi wanaita kundi kubwa kama vile majeshi, wanachuo na wananchi wakati wa utekelezaji wa zoezi upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali.
Alisema vifaa hivyo vitasaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa vifaa vya kusombea samadi, umwagiliani hata wakati wa upimaji maeneo ya kupanda miti hiyo.
Mwanri alitoa wito kwa Kampuni nyingine zinahusika na ununuzi wa tumbaku na zisizohusika na tumbaku mkoani humo kuona umuhimu wa kuunga mkono jitihada hizo za upandaji miti kwa kusaidia vifaa mbalimbali ikiwemo magari kwa ajili ya kumwagilia maji wakati wa kiangazi.
Alisema kuwa vikipatikana vifaa kwa wingi kazi kubwa itafanyika ya kuhakikisha miti inapandwa kwa wiki katika maeneo mbalimbali ili kurudi uoto wa asili na kuboresha mazingira mkoani humo.
Naye Mwenyekiti wa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Nathalis Linuma alimshukuru Kampuni kwa kuuwezesha Mkoa huo kupata vifaa hivyo ambavyo si tu vitatumika katika upandaji wa miti bali hata katika shughuli mbalimbali kama vile usafi wa mazingira.
Alisema kuwa watahakikisha wanatunza vifaa hivyo ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kuleta tija kwa Mkoa





0 Comments