Random Posts

Hatimaye Yanga kukutana na Enyimba ama Almasry ya Misri kombe la Shirikisho

Baada ya kutolewa na Township ya botswana hatimaye Yanga kudondokea kwa ENYIMBA ama Almasry.
Na George Mganga
Kufuatia kuangukia katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Jumamosi ya jana, Yanga inaweza ikapangiwa kucheza na vigogo kadhaa barani Afrika.
Bado haijapangwa kuwa Yanga itacheza na nani, ingawa timu zilizopo kwenye mashindano hayo mojawapo ni Enyimba FC kutoka Nigeria.
Si Enyimba pekee, baadhi ya timu zingine zinazoshiriki Kombe la Shirikisho ni Zamalek, Raja Cassablanca, SuperSport United ya Afrika Kusini na Al Masry ya Misri.
Vigogo Enyimba leo watakuwa na kibarua kucheza dhidi ya Energie FC. Katika mechi ya kwanza Enyimba alishinda jumla ya mabao 2-0.

Post a Comment

0 Comments