Random Posts

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Yakagua Ujenzi wa Ofisi za Uhamiaji Mkoani Mtwara.

 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakimsikiliza kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara (hayupo kwenye picha) akizungumza wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa katika kikao kilichofanyika Machi 19, 2018 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
 Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Salum Rehani akizungumza jambo wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa katika kikao kilichofanyika Machi 19, 2018 ofisini kwake Mkoani Mtwara.
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu (kushoto) akisalimiana na afisa uhamiaji Mkoa wa Mtwara, James Mwanjotile (kulia) wakati kamati hiyo ilipoenda kukagua ujenzi wa ofisi za uhamiaji Mkoa wa Mtwara  19 Machi, 2018 Mkoani Mtwara.
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu (kulia) akipokelewa na katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) wakati kamati hiyo ilipoenda kukagua ujenzi wa ofisi za uhamiaji Mkoa wa Mtwara  Machi 19, 2018 Mkoani Mtwara.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu (katikati) akisisitiza jambo pale kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa ofisi za uhamiaji Mkoa wa Mtwara Machi 19, 2018 Mkoani Mtwara.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Post a Comment

0 Comments