BARAZA la
Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tabora-Uyui limepitisha mapendekezo ya
marekebisho ya bajeti ya ruzuku ya miundombinu LGCDG ya bilioni 1.9 kwa ajili
ya mwaka huu wa fedha (207/18).
Mapendekezo ya
marekebisho ya bajeti hiyo yaliwasilishwa jana Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo Hadija Makuwani katika kikao cha dharura cha Baraza hilo.
Alisema wameamua kufanyika
marekebisho hayo kufuatia agizo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa za kuzitaka Halmashauri zote nchini kufanyia uchambuzi
upya bajeti za miradi ili kuwa na michache inayotekelezeka na kukamilika kwa
wakati na kwa asilimia 100.
Makuwani
aliongeza miradi iliyopitishwa baada ya marekebisho ni pamoja na ujenzi wa
madarasa 13 na majengo ya utawala matatu katika shule za Sekondari 6 ambayo
itagharimu milioni 365.
Miradi mingine
ni ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika shule za Sekondari Usagari na ujenzi
wa mabweni matano katika Shule za Sekondari ambayo itagharimu milioni 235.
Alitaja miradi mingine kuwa ni
ukamilishaji wa vyumba 10 vya mahabara katika Sekondari 10 ambapo wanatarajia
kutumia milioni 302.5.
Makuwani
alisema pia kutakuwepo na ujenzi wa madarasa 11 na ofisi za walimu 4 katika shule
za msingi ambao utagharimu milioni 190.
Mradi mwingine
ni ukamamilishaji wa jengo la wagonjwa wan je (OPD) na ujenzi wa wodi mbili za
wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ambapo watatumia milioni 300.
Makuwani
alisema sehemu ya fedha hizo zitasaidia katika kukamilisha Zahanati ya
Ishihimulwa ambapo milioni 70 zitatumika na ukamilishaji wa wodi ya wazazi
katika Zahanati ya Imalakaseko kwa milioni 80.
Fedha nyingine jumla milioni 300
zitatumika kwa ajili ya kununulia nyumba za Shirika la Nyumba kwa ajili ya
watumishi kuishi watumishi wa Halmashauri hiyo.
Makuwani
alisema uratibu na ufuatiliaji utatumia milioni 96.9.

0 Comments