Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tabora(RCC) jana wakati wa kupitia mapendekezo bajeti ya mwaka ujao wa fedha.(kulia) Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasubi na kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa Nathilis Linuma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tabora(RCC) wakiwa katika kikao cha kupitia mapendekezo ya mpango wa bajeti ya mwaka ujao wa fedha.Picha na Tiganya Vincent.
NA TIGANYA VINCENT RS-TABORA
MKOA wa Tabora umepitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti ya bilioni 296.2 kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mapendekezo hayo yamepitishwa Machi 2, 2018 na Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tabora.
Akiwasilisha mapendekezo ya bajeti hiyo Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Hajjat Rukia Manduta alisema kati ya fedha hizo bajeti ya Sekretarieti ya Mkoa(RS) ni bilioni 11.6 na Mamlaka ya Serikali za Mitaa(MSM) ni bilioni 284.6.
Alisema kati ya fedha hizo 203.3 ni mishahara, matumizi mengineyo ni bilioni 23.3 na miradi ya maendeleo bilioni 69.6 .
Hajjat Rukia alisema mwaka ujao wa fedha mapato ya ndani yatakuwa bilioni 35.8 na mishahara itakuwa bilioni 33.7.
Alisema kwa MSM bilioni 195.2 ni mishahara, matumizi mengineyo bilioni 21.6 , miradi ya maendeleo ni 67.7 ambapo fedha za ndani ni shilingi bilioni 34.4 na fedha za nje ni 33.2.
Hajjat Rukia alisema kuwa kwa upande wa RS mishahara ni bilioni 8, matumizi mengineyo ni bilioni 1.7, miradi ya maendeleo ni bilioni 1.8 na fedha za ndani ni bilioni 1.3 na fedha za nje ni milioni 536.3.
Aidha Katibu Tawala huyo Msaidizi alikizungumzia mapitio ya bajeti ya mwaka 2017/18 alisema Mkoa wa Tabora ulidhinishiwa kukusanya mapato ya jumla ya bilioni 239.3.
Aliongeza kuwa hadi kufikia Desema mwaka jana ulikuwa umeshapokea bilioni 105.2 ambazo ni sawa na asilimia 44.
Katika hatua nyingine Hajjat Rukia alizitaka Halmashauri kupanga kuwa miradi michache inayokamalika kuliko kuweka miradi mingi ambayo haikamiliki katika kipindi cha mwaka wa fedha husika.
Alisema kuwa hatua itasaidia miradi kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.


0 Comments