Random Posts

TACAIDS Yatoa Mafunzo kwa Wahariri Vyombo vya Habari juu ya kuandaa program bora za VVU na UKIMWI.



Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari na wahariri wa vyombo vya habari Mjini Bagamoyo ya Februari 6, 2018 juu ya kuandaa program bora za VVU na UKIMWI.

Ambapo amesema takwimu zinaonesha kila siku watanzania mia mbili ishirini na tano
hupata maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi ambapo maambukizi hayo
kwa mwaka hufikia elfu themanini na moja.

Amesema asilimia 40 ya maambukizi ya kila siku yanatokea kwa vijana wenye  umri kati ya miaka 15-24 ambapo katika kila maambukizo ya watu 10 kwa vijana hao maambukizi ya watu 8 ni vijana wa kike na 2 ni wa kiume.
Dkt. Maboko amebainisha kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha ifikapo 2030 Tanzania iwe imetokomeza kabisa maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI, kumaliza  vifo vitokanavyo na HIV pamoja na kuondoa unyanyapaa kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI ndani ya jamii.
Baadhi ya  waandishi wa habari na wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mafunzo juu ya kuandaa program bora za VVU na UKIMWI Mjini Bagamoyo  Februari 6, 2018 .
 Mtoa mada Charles Kayoka akielezea umuhimu wa mitandao ya kijamii kuweza kuandika na kushea habari wakati wa mafunzo hayo.
 Watoa mada wakiendelea kutoa mada.
 Mkurugenzi wa Uraghbishi na Habari  kutoka  Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDSBw.Jumanne Issango akitoa mada.
 Mkurugenzi wa Idara na Sera Mipango na Utafiti kutoka  Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Richard Ngirwa akielezea mkakati wa nne wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI 2018-2023 wakati wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akiwa kwenye picha ya pamoja na  wahariri na waandishi wa Habari  mara baada kufungua mafunzo juu ya kuandaa program bora za VVU na UKIMWI .Mjini Bagamoyo  Februari 6, 2018. 

PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON

Post a Comment

0 Comments