Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye, ofisini kwa Waziri Mkuu
mini Dodoma, Machi 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye, ofisini kwa Waziri Mkuu
mini Dodoma, Machi 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema ni umuhimu mfumo wa ufundishwaji wa
wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ukaboreshwa ili wanapomaliza waweze
kujiajiri.
“Kumekuwa
na tatizo kubwa la wasomi wetu kuwa na mtazamo kwamba wanapomaliza
masomo yao lazima waajiriwe. Upo umuhimu wa kubadili mtazamo huo kwa
kuwapa mbinu zitakazowawezesha kujiajiri.”
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Machi 16, 2018) alipokutana na
kufanya mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.
William Anangisye, ofisini kwake mjini Dodoma.
Amesema
wanafunzi hao wanapomaliza wanatarajiwa wawe na uwezo wa kubuni mbinu
mbalimbali za kujiajiri na kuondokana na mtazao wa kusubiri ajira za
kuajiriwa maofisini.
Waziri
Mkuu amesema wasomi hao wanaweza kuchukua kauli mbiu ya Rais Dkt. John
Magufuli ya uchumi wa viwanda kwa kuanzisha kilimo cha mazao mbalimbali
yatakayotoa malighafi za viwandani.
Pia
Waziri Mkuu amesema wasomi hao wanaweza kujikita katika shughuli za
uchimbaji wa madini au usindikaji wa mazao mbalimbali, hivyo tayari
watakuwa wamejiajiri kwa sababu ajira si za ofisini pekee.
Aidha,
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam aliyestaafu Profesa Rwekaza Mukandara kwa kazi nzuri
aliyoifanya kipindi cha uongozi wake.
Kwa upande wake, Profesa
Anangisye amesema mzigo aliopewa wa kuiongoza taasisi hiyo si mwepesi,
hivyo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na hatokwenda kinyume na matarajio
ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Kiongozi
huyo amesema katika kuhakikisha wanaboresha masomo chuo hapo
wameanzisha skuli ya kilimo na uvuvi, hivyo wanatarajia kuanzisha
mashamba ya mfano kwa ajili ya mazao mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980
IJUMAA, MACHI 16, 2018.
0 Comments