Mh. Ahamad Rashid Mohamed akipiga mpira ikiwa ni ushara ya kufungua tamasha la michezo ambalo linafanyika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Wachezaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (waliovaa jezi nyekundu) wakielekea katika lango la wapinzani wao.
Kutoka kushoto Mwalimu wa timu mpira wa pete, Mwajuma Kisengo, Mh. Ahamad Rashid Mohamed na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala (DHR) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makwaia Makani wakifuatilia tamasha hilo leo kwenye uwanja wa MUHAS.
Mshiriki kutoka timu ya Afya Zanzibar, Juma Haji Mlekwa, akichangia damu leo kabla ya kuanza kwa mpira wa miguu kati ya timu ya Afya Zanzibar na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).
Mwalimu wa mpira wa pete kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mwajuma Kisengo akichangia damu kabla ya kuanza kwa mpira wa miguu kati ya timu ya Afya Zanzibar na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)
…………………
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed leo amefungua tamasha la michezo ya Pasaka inayohusisha timu za michezo kutoka Wizara ya afya Zanzibar , Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) , Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) pamoja na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo Mhe. Hamad Rashid Mohamed amesema afya bora hujengwa na michezo hivyo amewataka viongozi kuendeleza michezo katika taasisi zao ili watumishi wawe na afya bora hatua itakayowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
‘’Ukiwa na afya bora hata hutendaji wako wa kazi utakuwa na ufanisi mkubwa hivyo nawasihi muendeleze michezo ili kuendelea kujenga taifa letu,’’ amesema Mh. Rashid.
Mbali na hilo lakini pia amesema katika historia ya nchi yetu michezo imekua kielelezo muhimu katika kudumisha undugu , umoja , mshikamo na muungano wetu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Bw. Makwaia Makani ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru , amesema Tamasha hilo la michezo hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu MNH ni wenyeji na mwakani iltafanyika Visiwani Zanzibar.
“Imekua utamaduni wetu kila mwaka kushiriki katika michezo hii kwa lengo la kuendeleza ushirikiano wetu wa muda mrefu ,pia niseme tu michezo ni kitu muhimu kwa mwanadamu kwani hutujenga afya na akili,’’ amesema Bw. Makani.
Tamasha hilo linahusisha mchezo wa mpira wa miguu na pete na pamoja na mambo mengine shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo zoezi la kuchangia damu na kusafisha maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Tamasha hilo limeanza leo na litamalizika Aprili 2 , 2018.






0 Comments