Random Posts

Waziri Mwakyembe amtaka Msanii Roma Mkatolilki kujisajili BASATA ili aweze kuendelea na shughuli za Sanaa

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari nakala ya cheti cha usajili cha msanii Pretty Kind kutoka BaASATA wakati wa kikao na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.

Na Genofeva Matemu – WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amemtaka Msanii wa muziki wa bongo fleva Roma Mkatoliki kujisajili BASATA ili aweze kuondolewa kwenye kifungo chake cha kutokufanya shughuli za sanaa kwa miezi sita alichofungiwa mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu.

Hayo ameyasema wakati wa kikao na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam baada ya kikao na wasanii wa mziki Roma Mkatoliki na Pretty Kind ambapo Wizara ilimtaka msanii Roma kubadilisha wimbo wake wa kibamia na kujisajili BASATA ili aweze kuondolewa katika kifungo hicho ambapo msanii huyo alitangaza kuufuta wimbo huo na kuahidi kujisajili BASATA ili aweze kuendelea na mziki.

“Kwa kuwa msanii Roma Mkatoliki ameamua kuufuta kabisa wimbo wa kibamia na kuvitaka vyombo vya habari kutokuucheza tena wimbo huo Wizara inamfungulia kifungo chake mara tu baada ya kujisajili BASATA atakuwa huru kuendelea na kazi zake za sanaa” amesema Mhe. Mwakyembe

Aidha Naibu Waziri Shonza amesema kuwa Msanii Suzan Michael (Pretty Kind) ametambua kosa alilolifanya na kukiri kosa hilo kwa kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuandika barua ya kuomba msamaa na kujisajili BASATA kuwa msanii halali hivyo Wizara kwa kushirikiana na BASATA imeridhia kumfungulia adhabu aliyopewa ya miezi sita ambayo kimsingi ilitakiwa kuisha tarehe moja julai mwaka huu. 

“Kuanzia sasa msanii Pretty Kind yupo huru kuendelea na kazi zake za sanaa kutokana na yeye kutimiza matakwa aliyoagizwa kuyafanya na kuahidi kuwa balozi mwema wa masuala ya maadili kwa wasanii wenzake” amesema Mhe. Shonza.

Post a Comment

0 Comments