Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI
imetenga kiasi cha sh.bilioni 39 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi
ambao maeneo yao yatapitiwa na mradi wa umeme mkubwa unaotarajiwa
kupitishwa kwenye maeneo yao.
Pamoja
na hilo ,baadhi ya miradi ya awali ambayo fidia imechelewa kwa walengwa
,uhakiki tayari umekamilika na utaratibu ukikamilika malipo yatafanyika
hivyo wananchi watoe shaka kwani serikali inataka ikabiliane na
ubabaishaji.
Hayo
yalisemwa na Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu alipokuwa
akizungumzia suala la fidia kwa baadhi ya wananchi watakaokuwa na haki
ya kupatiwa.
Alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na utagharimu fedha nyingi.
Subira
alielezea mradi unaanzia Rufiji, Kinyerezi,Kibaha na Chalinze na
baadaye Dodoma ambapo wananchi watalipwa wakati utakapoanza.
“Suala
la fidia ni kubwa na kwa ile miradi ya awali ambayo haijalipwa ni kweli
kwani baadhi bado hawajalipwa lakini wananchi wasiwe na wasi wasi kwani
watalipwa fidia zao mara uhakiki utakapokamilika,” alisema Subira.
Alielezea
,kwa bajeti ambayo inaendelea kwa sasa zimetengwa kiasi cha sh.bilioni
21 kwa ajili ya fidia kwa laini inayoanzia Kinyerezi, Kibaha, Chalinze
na Arusha ya umeme wa KV 400.
Kwa mujibu wa Subira,mradi huo ulifanyiwa tathmini 2014/2015 na fidia imechelewa hivyo serikali inaomba radhi kwa hilo.
"Serikali
ina majukumu na vipaombele mengi, haikusudii kuchelewesha bali mwaka
unaoendelea wa bajeti zitalipwa tu,” alisema Subira.
Aidha
alisema ,wakati Rais Dk. John Magufuli anaingia madarakani kulibainika
kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na wizi mkubwa kwenye suala la fidia
kwani walikuwa wakilipwa watu wasiostahili ambapo fedha inayopangwa na
serikali inabadilishwa na kuwekwa viwango vingine hasa inapofika ngazi
ya wilaya.
“Walikuwa
wanabadili watu wanaopaswa kulipwa wanabadilisha majina na kila kitu
hadi picha hata akilipwa anayestahili analipwa kiwango kisichotakiwa
hali iliyosababisha hazina kufanya uhakiki,” alifafanua.
Subira
alisema, uhakiki tayari umefanyika na utaratibu ukikamilika malipo
yatafanyika hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi licha ya kucheleweshewa
fidia zao bali serikali inataka iondokane na ubabaishaji.

0 Comments