Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa (CCM) Said Rubeya akikambizi
vifaa kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto kwa kununua mashine
mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu
(3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya
shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000) ili kuboresha maisha ya
wananchi wanaohudumiwa na hospital hiyo
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa (CCM) Said Rubeya akikambizi
vifaa kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto kwa kununua mashine
mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu
(3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya
shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000) ili kuboresha maisha ya
wananchi wanaohudumiwa na hospital hiyo
Baadhi
ya wananchi,makada wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa na viongozi wa
chama hicho waliokuwa wameudhulia makabidhiano ya vifaa kati ya uongozi
wa hospital na viongozi wa chama hicho manispaa ya Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA
cha mapinduzi manispaa ya Iringa kimetumia zaidi ya shilingi million
tano kuanza kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali ya
Frelimo iliyopo wilaya ya Iringa kwa kununua mashine mbili za kufulia na
televisheni moja aina ya LG nchi 43.
Akizungumza
wakati wa kukatibidhi vifaa hivyo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema kuwa hospital hiyo inakabiliwa na
changamoto nyingi hivyo wameamua kuanza kuzitatua kwa awamu na
kuangalia vipaumbele stahili.
“Tulikuja
kwenye ziara hapa na viongozi wangu na tulikutana na viongozi wa
hospatali hii wakatueleza changamoto nyingi sana ambazo ni ngumu
kutekeleza kwa siku moja hivyo tulitoka na vipaumbele vyetu sisi kama
chama ndio maana leo tumenza na hili na tutafuta na jingine” alisema
Rubeya
Awali
akisoma risala kwa mgeni rasmi mganga mfawidhi wa hospital hiyo, Dr
Pilila Zambi alisema kuwa hospital hiyo inakabiliwa na changamoto
zifuatazo jengo la vipimo na uchunguzi,wodi ya kulaza wagonjwa,wodi ya
watoto,wodi ya kulaza wagonjwa wa magonjwa ya kuambukiza,jengo la
utakasaji wa vifaa,jengo la kufulia nguo,nyumba za watumishi na ukosefu
wa uzio.
Aidha
Dr Zambi aliongeza kuwa hospital hiyo inaupungufu wa vifaa tiba ambavyo
vimekuwa vikikamisha shughuli za kutoa huduma bora kwa wananchi,vifaa
hivyo ni biochemistry machine,hematology machine Viral load
analyser,Ultrasound machine na X-ray machine.
“Tukipata
pia mashine kama mashine ya utakasaji, mashine ya kufulia na automatic
genereta basi hapo tutakuwa tumefanikiwa kutatua changamoto za hospitali
na tutatoa huduma bora kwa wananchi wanakuja kupata huduma katika
hospital hii” alisema Zambi
Rubeya
alisema kuwa kutokana na changamoto hizo ndio maana wameanza na kununua
mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi
milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye
thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000)
“Tuliona
tuanze na vifaa hivi vidogo kwasababu inasikitisha kuona kuwa nguo
chafu zenye vimelea vya magonjwa mbalimbali vinapitishwa katika ya mji
hadi hospital ya Rufaa hivyo tukaamua kutatua kwa hii changamoto, pia
wauguzi na madaktari mnatakiwa kujua nini kinaendelea nchi kwetu na nje
ya nchi hiyo tukaamua kuwaletea TV hii kwa ajili ya mafunzo mbalimbali”
alisema Rubeya
akizungumza kwa niaba ya mstahiki meya diwani wa kata ya mivinjeni Frank Nyalusi amewataka viongozi wote kuleta maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa na kuwashukulu viongozi wa chama cha mapinduzi kwa kuwafungulia njia ya maendeleo.
“Mimi
binafsi niwapongezee chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa mliyoifanya
hapa kwa kutusaidia kutatua changamoto za hospital hii” alisema Nyalusi
0 Comments