Balozi maalum wa DStv Khadija Kopa (Kushoto) akitia nakshi wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv NI MOTO’. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam ambapo pia DStv ilitangaza kuwa itarusha matangazo ya Kombe la dunia kwa lugha ya Kiswahili
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria (kulia) na mwenzake wa Masoko Salum Salum (Kushoto) wakionyesha ishara ya moto wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv NI MOTO’. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam ambapo pia DStv ilitangaza kuwa itarusha matangazo ya Kombe la dunia kwa lugha ya Kiswahili. Wengine (kutoka kulia) ni mabalozi wa DStv Khadija Kopa, Soudy Brown, Riyama Ally na Nancy Sumari.
* Matangazo ya Kombe
la Dunia kurushwa kwa Kiswahili
* Yaongeza Channel
maalum ya amsha-amsha ya Kombe la Dunia
Sasa mteja kutazama
DStv popote alipo kutumia App ya DStv Now.
Dar es Salaam Jumanne Aprili 24, 2018: Katika kuelekea msimu wa
kombe la Dunia 2018,
Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia king’amuzi chake cha
DStv imezindua kampeni mpya ifahamikayo kama DStv ni moto!
Mteja wa DStv sasa anaweza kujiunga na huduma iitwayo
“DStv Now” na kutazama vipindi vya DStv wakati wowote mahali popote ikiwa
ni pamoja na kupata fursa ya kuunganisha vifaa vitano (5) zaidi ikiwemo simu ya
kiganjani, Tablet, Laptop au Desktop pamoja na Runinga.
Hii inamaanisha watu wa
tano (5) tofauti wanaweza kutazama huduma ya DStv kupitia vifaa vitano (5)
tofauti kwa wakati mmoja na kwa akaunti moja tu ya malipo ya mwezi!
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaa
Jana, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Alpha Mria alisema “Wakati
tunaelekea kwenye mashindano makubwa kabisa ya soka Duniani yaani
Kombe la Dunia la FIFA , tunampa fursa mteja kutazama huduma ya DStv kwenye
vifaa hadi vitano kwa wakati mmoja.
Hii itawaondolea wateja
wetu usumbufu na sintofahamu hususani pale watu wengi wanapotaka kutazama vitu
tofauti wakati wowote mahala popote kwa wakati mmoja“
Aliongezea kusema “Tumekuwa tukiboresha huduma zetu kila uchao
hususan kuongeza maudhui na pia kuwarahisishia wateja wetu utazamaji wa vipindi
mbalimbali tena kwa kiwango cha hali ya juu kabisa“ alisema
Alpha na kuongeza kuwa App hiyo ya DStv Now inapatikana kwa
wateja wa vifurushi vyote.
Alpha amesema kwa kuzingatia uzito wa michuano ya Kombe la dunia
mwaka huu, DStv imejipanga kuhakikisha kuwa watanzania wanapata fursa ya kuona
mechi zote zikiwa katika mfumo wa HD, na pia kwa bei nafuu sana na kwa jinsi
watakavyo wateja.
“Kwanza tunakupa fursa ya kutazama kombe la Dunia popote
ulipo iwe ni kwenye laptop, tablet, simu, au kwenye runinga yako; ni chaguo
lako na ndiyo sababu tunasema Burudika popote ulipo na DStv.. DStv
ni moto!“
Pia amebainisha kuwa DStv itakuwa ikirusha matangazo ya michuano
hiyo kwa lugha ya kiswahili kwa kuwatumia watangazaji nguli wa michezo hapa
nchini.
Amesema kuwa kumekuwa na maombi mengi sana kutoka kwa wateja
kutaka matangazo hayo yarushwe kwa kiswahili hivyo DStv imetimiza matakwa ya
wateja wake na sasa itarusha matangazo hayo kwa Kiswahili.
Kujiunga na huduma ya “DStv Now”, mteja
anapaswa kupakua App ya DStv Now kupitia Simu yake ya mkononi au Tablet ama
Laptop na Desktop ataingia DStv.com kisha kufuata maelekezo na kisha kujisajili
kwa kuweka taarifa zake muhimu ikiwemo email (barua pepe) namba ya simu pamoja
na Smartcard number ya DStv.
Baada ya hapo mteja anaweza kufurahia huduma ya DStv wakati
wowote mahali popote. Huduma hii inapatikana kwenye vifurushi vyetu vyote vya
DStv.
Amewataka wateja wa DStv na watanzania kwa ujumla kukaa mkao wa
kula kwani kuna mambo makubwa sana kutoka DStv msimu huu wa kombe la Dunia.
“Huu ni mwanzo tu wa moto
wa Kombe la Dunia, siku chache zijazo tutasikia makubwa zaidi kutoka DStv
kuhusu mashindano haya “
Kama hiyo haitoshi, kuanzia April 18 mwaka huu, DStv iliongeza
chanel maalum DStv 214 inayopatikana kwenye vifurushi vyote, ambayo ni
mahususi kwa amsha-amsha za kombe la Dunia.
Channel hii huelezea historia na matukio muhimu ya Michuano hiyo
na pia kuonyesha mechi kadhaa za michuano iliyopita bila kusahau makala maalum,
mahojiano na wadau na wataalamu mbalimbali wa soka na matukio yote yaliyotikisa
michuano hiyo kwa miaka iliyopita.
Zaidi ya hayo, DStv inaendelea kukupa maudhui moto moto hasa
kipindi hiki cha kulekea msimu wa Kombe la Dunia, kwani utashuhudia fainali za
UEFA champions League, Fainali za Europa League, Fainali za FA Cup, Na mwisho
wa msimu wa Premier League na Laliga bila kusahau Filamu na Tamthilia kali za
kusisimua za ndani na nje ya nchi, WWE Mashindano ya Mieleka, vipindi vya
mapishi, watoto na vingine vingi, Hakika ni DStv NI MOTOOO!!
0 Comments