Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack
Kamwelwe akijibu hoja mbalimbali zilizobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
katika Wizara yake mjini Dodoma Aprili 18,2018 wakati wa mkutano na waandishi wa habari (
hawapo pichani).
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa Mawaziri wote kukutana na waandishi wa habari kujibu hoja mbalimbali zilizobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Wizara zao mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijibu hoja mbalimnbali zilizobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Ofisi hiyo mjini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso mapema leo mjini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliowashirikisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.

Upatikanaji wa maji
mijini na vijijini umeimarika kutoka chini ya 50% ya awali kutokana na umakini
katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji safi nchini.
Aidha, ili kukabiliana na mazingira Serikali imeanza mchakato wa kutumia mifumo
ya kisayansi ili kuondoa matumizi ya mkaa majumbani.
Hatua hizo zimebainishwa
leo na Mhe. Isack Kamwelwe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mhe. Januari
Makamba, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira)
walipokuwa wakieleza utekelezaji wa hoja za CAG katika sekta zao.
Akizungumzia hoja kuhusu
utekelezaji wa miradi ya maji nchini, Waziri Kamwelwe amesisitiza kuwa tangu
Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, ufuatiliaji na kuzibwa mianya ya
ubadhirifu vimeleta mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji
mijini na vijijini.
“Sisi kwa upande wetu
CAG anatuonesha njia ili tufanye vizuri zaidi. Hadi kufikia Desemba, 2017,
upatikanaji wa maji mijini umepanda hadi kufikia asilimia 78. Kwa upande wa
vijijini, hadi kufikia Machi 2018, Serikali kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali, imejenga vituo vya kuchotea maji 123,888 vyenye uwezo wa kuhudumia
takribani watu milioni 30 sawa na asilimia 68.8,” alisema.
Kwa upande wake, Waziri
Makamba amesema hoja za CAG zimewasaidia kuongeza mikakati hasa ya kutumia
sayansi na teknolojia kupata mbadala wa matumizi ya mkaa ili kuokoa misitu na
kutunza mazingira. Amesema tayari Ofisi yake na wadau wanafanya majaribio ya
baadhi ya teknolojia hizo.
Kuhusu changamoto za
kupambana na taka za kielektroniki, amekiri kuwa Tanzania kama nchi nyingine
zinazoendelea inakumbana na changamoto ya kupokea vifaa vingi vilivyotumika
kama kompyuta, simu na chaja ambavyo huharabika haraka na kutupwa kama taka za
kielectroniki.
“Ofisi ya Makamu wa Rais
imeanza kutoa vibali kwa makampuni 16 yenye utaalamu kwa ajili ya kukusanya,
kusafirisha na kurejeresha (recycling) taka za kielektroniki,” alisema.

0 Comments