Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa Tawi la CCM Mtende Mndo, Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.
Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Mkoa Kusini Unguja kusema pale
wanapoona Viongozi wao hawafanyi yale walioyaahidi badala ya kulalamika chini
kwa chini na kuwapongeza pale wanapotimiza ahadi zao.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa
ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais aliwaambia wakazi wa mkoa wa
kusini Unguja kutouza ardhi kiholela na kuyatunza mazingira.
Makamu wa Rais amewaambia wananchi wa Mkoa
wa Kusini Unguja kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuleta mabadiliko
makubwa hasa kwa mkakati wa kuifanya nchi kuwa na Uchumi wa Viwanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Katibu wa Chadema mkoa wa Kusini Unguja Bw. Ali Othman Shomari ambaye amejiunga na CCM leo wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Mtende Mndo, Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)




0 Comments